SoC03 Tuielimishe jamii umuhimu wa kuyatunza Mazingira ili mazingira yatutunze

SoC03 Tuielimishe jamii umuhimu wa kuyatunza Mazingira ili mazingira yatutunze

Stories of Change - 2023 Competition

Chu joe

Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
7
Reaction score
3
Tarehe 5 ya mwezi Juni kila mwaka dunia huadhimisha siku ya mazingira duniani, lengo kuu la kuadhimisha siku hii ni kufahamu kwa undani umuhimu wa kutunza na athari zinazotokana na uharibifu wa mazingira.

Kwanza kabisa mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyomzunguka binadamu au kiumbe hai, mfano mito, bahari, maziwa, miti, majengo, misitu, milima mabonde, nk.

Zipo athari nyingi zinazotokana na uharibifu wa mazingira katika dunia yetu, mfano kuharibu tabaka la ozoni linalochangia ongezeko la joto, kuongeza hatari ya magonjwa ya mlipuko kwa kutupa taka ovyo mfano kipindupindu, na malaria kwa kutosafisha mazingira.

Leo nataka nizungumzie umuhimu wa kutunza mazingira ili tuweze kuilinda jamii dhidi ya athari zinazotokana na uharibifu wa mazingira kama kukata miti ovyo, kutupa taka bila mpangilio, kuharibu vyanzo vya maji, na kuchoma misitu.

Kuepuka magonjwa ya mlipuko, katika jamii yetu hapa Tanzania magonjwa ya mlipuko mfano kipindupindu na malaria yameendelea kuwatesa watu wengi huku wizara ya afya ikishindwa kumaliza tatizo hilo kutokana na uelewa mdogo wa wananchi juu ya maradhi hayo, yanayosababishwa na uchafuzi wa mazingira kutokana na kutupa taka ovyo na kutofanya usafi.

Kuokoa vyanzo vya maji, katika maeneo mengi nchini uhaba wa maji unatokana na uharibifu wa vyanzo hivyo mfano chemichemi, mabonde, na mito inayosambaza maji sehemu mbalimbali, kwahiyo tukiaacha kufanya uharibifu katika maeneo hayo tutamaliza tatizo hilo na kupeleka maji kupatikana ya kutosha kwaajili ya matumizi ya majumbani, viwandani nk.

Kupata umeme wa uhakika na wa kutosha, nchini Tanzania tunategemea umeme unaozalishwa kutoka katika mabwawa tofauti mfano bwawa la nyumba ya Mungu, na bwawa la Nyerere, mabwawa hayo yote yanazalisha umeme kutoka katika vyanzo vya maji hivyo basi tukiyatunza mazingira tutapelekea kupata umeme wa uhakika na kupunguza tatizo la mgao wa umeme.

Kupata mazao ya kutosha, wakulima wengi wa mazao ya chakula na biashara wanategemea maji kwaajili ya kumwagilia mazao mashambani, na endapo maji yatakosekana na mvua isinyeshe basi mazao yatakauka kwahiyo ili kuepukana na hasara ya mimea kukauka shambani au mazao kupatikana kwa uchache ni lazima tutunze vyanzo vya maji na mazingira kiujumla.

Kupata hewa safi na upepo mzuri, watu wengi hupendelea kwenda maeneo yenye hewa safi na upepo mzuri ili kutuliza akili, kujiliwaza na kutafakari mambo mbalimbali, kwahiyo tunapoyatunza mazingira tunapata faida nyingi za kupata maeneo tofauti ya kupumzika hivyo basi tunapaswa kuendelea kutunza mazingira Ili yatutunze.

Kutunza uoto wa asili, tukiacha kuchoma miti hovyo tutasaidia kulinda uoto wa asili mfano misitu, mbuga za wanyama, hifadhi za taifa nk. ambazo tumerithishwa ili na sisi tuwarithishe vizazi vijavyo kwahiyo Kuna umuhimu mkubwa kutunza mazingira hasa mbuga za wanyama kwasababu ni moja ya njia za kuiingizia serikali fedha za kigeni.

Zipo faida nyingi na hizo nilizoorodhesha ni kwa uchache tu, lakini yote Kwa yote utunzaji wa mazingira unafaida nyingi kwa binadamu na viumbe hai wote wanaoishi katika dunia kwahiyo tukiyatunza mazingira na yenyewe yatatutunza.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom