SoC01 Tuiendeleze Tanzania yenye asili yetu, kwa kuendana na kasi ya Teknolojia

SoC01 Tuiendeleze Tanzania yenye asili yetu, kwa kuendana na kasi ya Teknolojia

Stories of Change - 2021 Competition

Mangwana

New Member
Joined
Jul 30, 2021
Posts
1
Reaction score
1
Tanzania ni nchi tajiri na yenye amani kubwa inayopaswa kutunzwa na kuendelezwa. Utajiri huu unatokana na rasilimali tulizonazo Kama vile Madini, watu, Wanyama na vinginevyo.

Uendeshwaji na matumizi ya rasilimali hizi unapaswa kushirikisha wananchi ambao ni wadau muhimu wa maendeleo.

Malumbano na mivutano ya kichama, kidini na kiutamaduni hayatatupa tija yeyote. Hivyo tunatakiwa kuwa wamoja katika kuijenga Tanzania Bora.

Kupanuka kwa TEKNOLOJIA kusitufanya tukaacha asili yetu Kama watanzania, tukaacha kupendana, kutengeneza makundi, kutoa taarifa za kupotosha na kuchochea jambo Fulani kwakuwa una uhuru wa kutuma taarifa mtandaoni, HAVITATUJENGEA TAIFA BORA Bali TUNAPOTOKA.

Kipato Cha raia kinategemea atoke nje ndio apate kula, hivyo tupambane na kujilinda na CORONA wakati tunajua uchumi wa nchi yetu na wa raia wetu.

Serikali inapaswa kuweka usawa kwa wananchi wote. Maana nchi ni ya kwetu sote na wachache ndio tumewapa mamlaka ya kutuongoza, vyama vya upinzani navyo vina haki kikatiba kuwepo, vinatakiwa vilete changamoto chanya kwenye kukosoa utendaji kazi wa viongozi kwa manufaa ya Taifa.

Janga la kupanda kwa bei za bidhaa linaumiza mwananchi wa chini. Umaskini unapaswa kupigwa vita na kila mwananchi, na tunatakiwa kukabiliana nao kwa kujituma kufanya kazi.

Mwisho naishauri Serikali kwenye upande wa elimu kuwa ili tuijenge tanzania yenye asili yetu, mafunzo ya ufundi yarudishwe kwenye elimu na mitaala ilenge kufundisha maisha halisi ya Tanzania ili kukwepa tatizo la kukosekana kwa ajira na kuwa na elimu isiyotusaidia.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom