SoC03 Tuifanye Elimu iwe Nuru

SoC03 Tuifanye Elimu iwe Nuru

Stories of Change - 2023 Competition

UziEXP

New Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
1
Reaction score
2
UTANGULIZI.
Elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii yoyote kiuchumi, kijamii pamoja na kisiasa. Maendeleo yoyote ya jamii hutegemea na kiwango cha ubora wa elimu tolewa nchi husika, kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusiana na ubora wa elimu tolewa yakwamba haina ubora huku baadhi ya wadau wakilalamikia kuhusu matumizi ya lugha ya kigeni kwenye mitahara ya elimu imepelekea kuzorota nakushuka kwa ubora wa elimu Tanzania pia baadhi ya wadau wakishauri kuwapo kwa mahojiano ya kazi kwa walimu ili kusudi kuweka walimu wenye sifa pendekezwa kwenye mfumo. Mbali na mikakati hii iliyopendekezwa matatizo ya elimu bado yameonekana kuwa na ukubwa na kuota usugu.

CHANGAMOTO.

Kushuka kwa ufaulu na ufanisi wa elimu kwa kuzalisha wasomo wengi wanaoshindwa kuona fursa ndani ya jamii. Uwepo wa mazingira duni ya upatikanaji wa walimu wa shule za umma umesababisha kupatikana kwa jopo kubwa wasio wajibika juu ya kazi yao pasipo hofia kitu chochote hivyo umefanya ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi katika shule za umma kuwa ni jambo ngumu ukilinganisha na taasisi binafsi za elimu pia mitahara imeshindwa kuwa na uhalisia na maisha ya mtanzania.

Kuongezeka kwa wanafunzi wanao tumia dawa za kulevya mashuleni hususani matumizi ya bangi yameonekana kukidhiri kwa baadhi ya shule huku tatizo hili likipewa njia duni katika kutatua chanzo chake. Wanafunzi wamekuwa wakijihusisha na masuala haya ya matumizi ya bangi kwa sababu mbalimbali kama vile kufeli mitihani, mazingira mabaya ya nyumbani kimalezi, na namna atunzwavyo pindi anapokuwa shuleni.

Kukosekana kwa msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi, limekuwa ni jambo mbaya na nikitu ambacho kimepelekea wimbi kubwa la wanafunzi kudumbukia katika matendo yasiyo kuwa na afya katika maendeleo ya kielimu pamoja na kimwili.

Visa vya mimba bado ni changamoto. Kesi za mimba kwa wanafunzi zimekuwa zikisikika jamii huku wahusika wakiwa ni ndugu jamaa wa karibu kitu ambacho hupelekea baadhi ya kesi kufunikwa chini ya kapeti lakin kuna baadhi ya matukio yamewataja walimu pia kama ni chanzo cha mimba hizi kwa wanafunzi jambo ambalo humletea mwanafunzi matatizo ya kisaikolojia sababu ya umri mdogo wakuweza kuyachambua mambo.

NINI KIFANYWE?

Upimaji wa Afya ya akili kwa walimu. Nje ya kuangalia kigezo cha ufaulu wa mwalimu anae omba ajira pia serikali haina budi kuandaa mikakati dhabiti kuhakikisha wanawapata wataalamu wa Afya ya akili " therapist " kuwapima walimu wote walio fuzu kwa kigezo cha ufaulu wa darasani , kwa kufanya jambo hili litaongeza ufanisi kwenye sekta ya elimu na kuondokana na kesi ambazo walimu wamekuwa walengwa katika kudidimiza ustawi wa wanafunzi na pia tukiwa tunatambua mwanafunzi hutumia mda mwingi na walimu wake kuliko mda anao tumia na wazazi wake hivyo uhakikishwaji wa usalama wa mtoto kwenye mikono ya walimu huwa ni wa hari ya juu. Mfano tumeshuhudia baadhi ya walimu wakiwapa adhabu watoto aidha ya fimbo au kazi ambazo haziendani na umri wao au aina ya kuadhibu mfano wa kupiga mwizi vitendo hivi nivigumu kufanyika kwa mwalimu alie na afya ya akili timamu kwa kutambua moja kwa moja vinaweza leta umauti au matatizo yakiakili kwa mwanafunzi aliye patwa na kazia hii.

Utolewaji wa mafunzo ya kitaalamu ya ushauri wa wanafunzi; kukosekana kwa walezi wa wanafunzi wasio kuwa na utaalamu katika kushauri wanafunzi limekuwa nitatizo katika shule zetu na hata ushauri ukitoka Mara nyingi huwa katika hatua ya mwisho ambayo mlengwa anakuwa ameathirika kwa hari ya juu. Kwenye nyanja hii ya elimu ushauri wa kitaalamu kwa wanafunzi ni jambo la msingi, Uwepo wa mwalimu wa kisaikolojia atakaye saidia wanafunzi pindi tu wanapo ripoti shuleni utasaidia kutatua matatizo na kadhia mbalimbali ambazo Wenda zisipo tatuliwa huwaweka vijana katika hari mbaya kitabia mfano, Ongezeko la ushoga limekuwa likitajwa kuonekana pia kwa wanafunzi huku likiwa na visababishi kadha wa kadha kama vile vitendo vya ulawiti wa watoto ambavyo hufanywa aidha mazingira ya nyumbani au Nje ya nyumbani kwa kuwa na washauri wataalamu wa saikolojia wataweza kuwapa msaada wanafunzi walio wahi pitia kadhia hii nakuweza kupunguza matokea hasi yakujiingiza kwenye tabia hizi chafu kabla hazijakomaa kwa mtoto.

Mwisho: Hakutakuwa na maana ya kuwekeza matrillioni ya pesa kwenye sekta itakayo zaa vilema wabadae , sekta inayo andaa tegemezi katika jamii , Sekta itakayo punguza nguvu kazi ya jamii. Jicho la pili lenye uzito halina budi kuchukuliwa nakuachana na kufanya mambo kwa mazoea Bali mifumo ya elimu inabidi iboreshwa kwa kiasi kikubwa kwa kuangalia maendeleo ya mtanzania yaleo nayajayo kwa kuifanya elimu iwe nuru kwa watanzania dhidi ya viongozi wasio na maadili na wasio tambua utu wa mtanzania.
close-up-idea-concept_1688884227307.jpg
 
Upvote 3
UTANGULIZI.
Elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii yoyote kiuchumi, kijamii pamoja na kisiasa. Maendeleo yoyote ya jamii hutegemea na kiwango cha ubora wa elimu tolewa nchi husika, kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusiana na ubora wa elimu tolewa yakwamba haina ubora huku baadhi ya wadau wakilalamikia kuhusu matumizi ya lugha ya kigeni kwenye mitahara ya elimu imepelekea kuzorota nakushuka kwa ubora wa elimu Tanzania pia baadhi ya wadau wakishauri kuwapo kwa mahojiano ya kazi kwa walimu ili kusudi kuweka walimu wenye sifa pendekezwa kwenye mfumo. Mbali na mikakati hii iliyopendekezwa matatizo ya elimu bado yameonekana kuwa na ukubwa na kuota usugu.

CHANGAMOTO.

Kushuka kwa ufaulu na ufanisi wa elimu kwa kuzalisha wasomo wengi wanaoshindwa kuona fursa ndani ya jamii. Uwepo wa mazingira duni ya upatikanaji wa walimu wa shule za umma umesababisha kupatikana kwa jopo kubwa wasio wajibika juu ya kazi yao pasipo hofia kitu chochote hivyo umefanya ufuatiliaji wa maendeleo ya wanafunzi katika shule za umma kuwa ni jambo ngumu ukilinganisha na taasisi binafsi za elimu pia mitahara imeshindwa kuwa na uhalisia na maisha ya mtanzania.

Kuongezeka kwa wanafunzi wanao tumia dawa za kulevya mashuleni hususani matumizi ya bangi yameonekana kukidhiri kwa baadhi ya shule huku tatizo hili likipewa njia duni katika kutatua chanzo chake. Wanafunzi wamekuwa wakijihusisha na masuala haya ya matumizi ya bangi kwa sababu mbalimbali kama vile kufeli mitihani, mazingira mabaya ya nyumbani kimalezi, na namna atunzwavyo pindi anapokuwa shuleni.

Kukosekana kwa msaada wa kisaikolojia kwa wanafunzi, limekuwa ni jambo mbaya na nikitu ambacho kimepelekea wimbi kubwa la wanafunzi kudumbukia katika matendo yasiyo kuwa na afya katika maendeleo ya kielimu pamoja na kimwili.

Visa vya mimba bado ni changamoto. Kesi za mimba kwa wanafunzi zimekuwa zikisikika jamii huku wahusika wakiwa ni ndugu jamaa wa karibu kitu ambacho hupelekea baadhi ya kesi kufunikwa chini ya kapeti lakin kuna baadhi ya matukio yamewataja walimu pia kama ni chanzo cha mimba hizi kwa wanafunzi jambo ambalo humletea mwanafunzi matatizo ya kisaikolojia sababu ya umri mdogo wakuweza kuyachambua mambo.

NINI KIFANYWE?

Upimaji wa Afya ya akili kwa walimu. Nje ya kuangalia kigezo cha ufaulu wa mwalimu anae omba ajira pia serikali haina budi kuandaa mikakati dhabiti kuhakikisha wanawapata wataalamu wa Afya ya akili " therapist " kuwapima walimu wote walio fuzu kwa kigezo cha ufaulu wa darasani , kwa kufanya jambo hili litaongeza ufanisi kwenye sekta ya elimu na kuondokana na kesi ambazo walimu wamekuwa walengwa katika kudidimiza ustawi wa wanafunzi na pia tukiwa tunatambua mwanafunzi hutumia mda mwingi na walimu wake kuliko mda anao tumia na wazazi wake hivyo uhakikishwaji wa usalama wa mtoto kwenye mikono ya walimu huwa ni wa hari ya juu. Mfano tumeshuhudia baadhi ya walimu wakiwapa adhabu watoto aidha ya fimbo au kazi ambazo haziendani na umri wao au aina ya kuadhibu mfano wa kupiga mwizi vitendo hivi nivigumu kufanyika kwa mwalimu alie na afya ya akili timamu kwa kutambua moja kwa moja vinaweza leta umauti au matatizo yakiakili kwa mwanafunzi aliye patwa na kazia hii.

Utolewaji wa mafunzo ya kitaalamu ya ushauri wa wanafunzi; kukosekana kwa walezi wa wanafunzi wasio kuwa na utaalamu katika kushauri wanafunzi limekuwa nitatizo katika shule zetu na hata ushauri ukitoka Mara nyingi huwa katika hatua ya mwisho ambayo mlengwa anakuwa ameathirika kwa hari ya juu. Kwenye nyanja hii ya elimu ushauri wa kitaalamu kwa wanafunzi ni jambo la msingi, Uwepo wa mwalimu wa kisaikolojia atakaye saidia wanafunzi pindi tu wanapo ripoti shuleni utasaidia kutatua matatizo na kadhia mbalimbali ambazo Wenda zisipo tatuliwa huwaweka vijana katika hari mbaya kitabia mfano, Ongezeko la ushoga limekuwa likitajwa kuonekana pia kwa wanafunzi huku likiwa na visababishi kadha wa kadha kama vile vitendo vya ulawiti wa watoto ambavyo hufanywa aidha mazingira ya nyumbani au Nje ya nyumbani kwa kuwa na washauri wataalamu wa saikolojia wataweza kuwapa msaada wanafunzi walio wahi pitia kadhia hii nakuweza kupunguza matokea hasi yakujiingiza kwenye tabia hizi chafu kabla hazijakomaa kwa mtoto.

Mwisho: Hakutakuwa na maana ya kuwekeza matrillioni ya pesa kwenye sekta itakayo zaa vilema wabadae , sekta inayo andaa tegemezi katika jamii , Sekta itakayo punguza nguvu kazi ya jamii. Jicho la pili lenye uzito halina budi kuchukuliwa nakuachana na kufanya mambo kwa mazoea Bali mifumo ya elimu inabidi iboreshwa kwa kiasi kikubwa kwa kuangalia maendeleo ya mtanzania yaleo nayajayo kwa kuifanya elimu iwe nuru kwa watanzania dhidi ya viongozi wasio na maadili na wasio tambua utu wa mtanzania.View attachment 2682778
Safi sana bwana kwa andiko lako
 
Back
Top Bottom