Tuifanye Kariakoo iwe ya Kisasa

mconservative

New Member
Joined
Aug 18, 2016
Posts
3
Reaction score
8
Karikaoo ni soko linalokutanisha watu wengi kutoka ndani na nje ya nchi na ndo sababu kuu likapewa hadhi yakuwa soko la kimataifa lakini ukweli ni kwamba mazingira na namna biashara zinavyoendeshwa ninachelea kulipa hadhi yakuwa ni soko la kimataifa. Ukiangalia miundo mbinu na namna biashara zinavyoendeshwa utagundua kuwa kunakitu hakipo sawa, barabara ambazo zilitakiwa zitumike kama access road kwa ajili yakwenda kufata bidhaa madukani zinatumika kama maduka ya machinga yani vurugu vurugu,

Naishauri Serikali izihamishe zile shule za pale K/koo -Benjamin sec wajenge soko kubwa lenye hadhi ya kimataifa angalau floor tatu au nne kwenda chini na majengo kadhaa juu yawe ni kwa ajili stoo na mahotel na rectional buildings, wajenge station kubwa underground (subway)Train itakayo kuwa na direct line angalau tatu zitakazo connect Bandari, Airport na Magufuli bus station.

Soko hilo litoe space kwa wafanya biashara kuwa na maduka makubwa yenye hadhi za kimataifa na zifanye kazi 24 hrs halafu huku juu tuache ibaki kuwa soko la wafanyabiashara wadogo wadogo na hao nao wakae katika mpangilio maalumu sio kukaa barabarani tunaonekana kama nchi ambayo hatuheshimu sheria na mipango yetu wenyewe, tunajenga barabara badala kutumia kama njia tunatumia kama masoko.
 

Mshauri Hangaya aongee na wajomba zetu, Dubai world waijenge kariakoo, halafu waiendeshe wao kwa miaka 1000, bila kulipa kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…