Tuimbe nyimbo za watoto(zamani)

Nimeamua kupitia tu hizi nyimbo nimejikuta narudi miaka ya 80.Aisee utoto wetu ulikuwa mzuri sana,nashangaa siku hizi hata ile michezo ya zamani ya kitoto imepotea kabisa.Watoto wetu wanacheza video games tu.
 
Kila kizazi na lwake. Na kila kizazi kilichotangulia kinalalamikia kizazi kipya. Hata hawa wacheza video games nao wakati wao ukifika wataanza kulalamikia kizazi kipya kuwa kiko legelege. Maisha yanaendelea...
 
Hii ndio a a a a, ina mkia mrefu a a a a.... Hii ndio e e e e e iko kama kata e e e e.... hii ndio iiiiiiiI ina kofia kichwani iiiiiiii.... hiii ndio o o o o iko kama yai o o o o.... hii ndio u u u u u u iko kama kikombe u.u u.u u
Then hapo tulikuwa tukiitikia aaaaaaaa kwa sauti kubwa
 
Swadiiina Swadiiina, nampenda Swadina Swadina Swadina, mama yake namjua namjua namjua, anauza vitumbua vitumbua vituumbua, tak* moja kaungua kaungua kaungua.....
Kama karatasi pepea, kama nailoni yayuka kama unanguvu.. Sogeaa.. Hahaha...
 
Daah...hii nyimbo kipindi hiko mchezo wa Tausi ndo unabambaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…