Tuimbe nyimbo za watoto(zamani)

Hii ndio a a a a, ina mkia mrefu a a a a.... Hii ndio e e e e e iko kama kata e e e e.... hii ndio iiiiiiiI ina kofia kichwani iiiiiiii.... hiii ndio o o o o iko kama yai o o o o.... hii ndio u u u u u u iko kama kikombe u.u u.u u
 
Asiyependa shuleee,ni mjinga kabisa,asiyependa shulee,ni mjinga kabisa.Baaarua ikija,haitembeza kutwa,baarua ikija haitembeza kutwa.Huyo huyoooo ni mjinga kabisa!
Kipindi hikobla kwanzaaa
 
Watoto zangu nyie, eeeee
Mimi mama yenu, eeee
Sina nguvu tena, eee
Ya kumuua simba, eeee
Simba ni mkali, eee
Alimuua baba, eee
Akamuua shangazi, eee
akamuua mjomba, eee
Akamuua bibi, eee
akamuua babu, eee
Haidhuru kimbieniiii
 
Mwaka 30 nalipata homa
Mganga ni jirani baba alimwita
akapewa kuku na shilingi sita
ooh mganga mjanja we mganga
tunatoa pesa na unatudanganya.
 
Nipeleke wapi kwa bakheresa
Kwa bakheresa kuna nn
Mwajuma katobolewa
Katobolewa na nani
Mangi muuza duka
Daa Mwajuma
Shilingi imemponza
Watu kumi na mbili
Midizini wamem..............
 
Babaa na Mamaa walifunga harusi chumbani....!
Kinyuli nyulikaaa..
Baishoo i love u baby....ila huu wa kike.
 
Bibi kilemba umelala wapi
Nimelala kwa selemani mpasua mbao
Umekula ninii?
Nimekula kitamu tamu kama sukali
Geuka nyuma naona hatari
Milima ya kwetu ina majabari...
 
NAMTAFUTA MKE WANGU
NAMTAFUTA MKE WANGU
HAPA HAYUPO
HAPA HAYUPO
KAENDA WAPI
KAENDA WAPI
KAENDA KUSUKA
KAENDA KUSUKA
CHANUO KAMPA NANI
CHANUO KAMPA NANI
SISI HATUJUI
SISI HATUJUI
HUU MTI GANI
WA MCHONGOMA
NIKIUKATA
HAUKATIKI
HATA KWA PANGA
HAUKATIKI
 
Tweeende tukawinde leeeo,
Tukawinde vipepeooo,
Aiii mama kipepeooo kipepe,
Aiii mama kipepeooo kipepe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…