SoC04 Tuinue adubini zetu kuichungulia Kariakoo kwa jicho la kiuchumi, ili kuongeza mapato na kuibua fursa mpya

SoC04 Tuinue adubini zetu kuichungulia Kariakoo kwa jicho la kiuchumi, ili kuongeza mapato na kuibua fursa mpya

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Feb 1, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Kariakoo ni soko kubwa Afrika mashariki na kati kutokana na haswa ikichagizwa na ubora wa bandari yetu ya Dar es salaam kupitisha asilimia kubwa ya mizigo yote kwa Afrika mashariki na kati.

Soko hili lina zaidi ya wafanyabiashara elfu arobaini (40,000) ambao ni jumla na rejareja, jambo ambalo limefanya mamlaka ya mapato kulifanya eneo hilo kuwa Mkoa wa kikodi.

Soko hili kila mwezi lina wastani wa kuingiza mapato Serikalini kuanzia billion 12 hadi billion 14, wastani wa 300,000-350,000 Tsh kwa kila mfanyabiasha kwa mwezi.

Licha ya tija hizo lakini kiuchumi soko hili limeshindwa kupiga Kwa kasi hatua stahiki kutokana na sababu mbalimbali, na hili linapelekea kupotea kwa mapato mengi ambayo yangefanya namba za makusanyo kuongezeka.

Katika suala la kuongeza mapato katika Mkoa wa kikodi wa Kariakoo ni lazima serikali ijitoe mhanga kuimarisha mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara ili kuwafanya wavutiwe na kulipa kodi bila kulazimishwa au kutengenezewa shinikizo.

Udadisi wangu kwa jicho la kiuchumi unabainisha changamoto zilizopo ambazo upelekea misuguano kati ya serikali na wafanyabiashara hadi wakati mwingine kuwepo migomo na migogoro ya mara kwa mara ni kama ifuatavyo:

•Eneo la kariakoo haliwezi tena kupokea wafanyabiashara wapya, inapelekea kuongezeka kwa wamachinga wengi barabarani swala linalopelekea migogoro kati ya wafanyabiashara wenye maduka na wamachinga wanaopanga bidhaa mbele ya maduka hayo.

• Kutokuwepo na usalama wa kutosha kwa raia na mali zao kutokana na msongamano mkubwa wa watu, kunaongeza hofu kwa wafanyabiashara wanaotoka Nchi jirani, ambapo kuna wakati matapeli na vibaka wamekuwa kero.

• Miundombinu kutokuwa na ubora stahiki, mfano, maegesho,barabara za kuingia mjini kuwa nyembamba , pia kujaa maji taka kwenye baadhi ya Mitaa hasa kipindi cha mvua mfano, kero maarufu eneo la jangwani kujaa maji na kupelekea njia kadhaa kutopitika.

Pia baadhi ya miundombinu ya umeme kuchoka, jambo ambalo utajwa kupelekea majanga mbalimbali ikiwemo miliopuko ya moto kutokea mara kwa mara na kuharibu biashara na mali za watu.

•Mamlaka ya mapato kutokutumia weledi ipasavyo kwenye ukusanyaji mapato, na badala yake kutumia nguvu na kutengeneza mazingira ya kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara. Udadisi wangu unabaini wakati mwingine mazingira ya aina hiyo upelekea kufanyika makadirio yasiostahili na kupelekea upotevu wa mapato mengi.

•Kukosekana kwa maghara ya kuhifadhia mizigo yanayotambulika, hili linapelekea wafanyabiashara kuficha mizigo yao na kuweka mizigo kidogo kwenye maduka yao, ikiwa lengo haswa ni kuweza kukadiliwa Kodi kidogo.

• Kutokuwepo utaratibu rafiki bandarini, na kuwepo kwa kodi 'chechefu' kwa wafanyabiashara pindi wanapotoa mizigo yao bandarini hali ambayo inapelekea kutoza mzigo mmoja Kodi zaidi ya mara mbili, jambo ambalo uongeza hisia hasi kwa wanyabiashara kuingia kwenye misuguano na mamlaka au wakati mwingine kubuni mbinu za kukwepa kodi ili kufidia.

IMG-20240629-WA0033.jpg

Chanzo: Mwananchi digital

Katika kukabiliana na hayo kwa uchanya, nini kifanyike?


• Serikali lazima ijielekeze kwenye uboreshaji wa miundombinu yote inayoingia mjini kama vile kuboresha barabara ili zipitike kwa ufanisi bila kuleta kero , kupambanua kwa ufanisi maeneo ya maegesho ili kuepusha swala la msongamano pamoja na kuweka mkakati unaosisitiza kuondoa tatizo la maji taka kujaa kipindi cha mvua au watu kuyafungulia kinyume na utaratibu.

•Ni muhimu Serikali iboreshe miundombinu ya umeme ili kuondoa uwezekano wa kutokea kwa majanga ya moto mara kwa mara, mfano kuondoa au kusisitiza wamiliki wa miundombinu kuziondoa nyanya za umeme zote zilizochoka na vifaa vingine ambavyo vimepitwa na wakati au kukosa ubora wa kuhimili mahitaji.

•Serikali kupitia mamlaka ya mapato Tanzania itoe elimu zaidi kwa maafisa wake kuweza kukusanya Kodi Kwa weledi zaidi na siyo kutumia mabavu au kukiuka misingi ya utawala bora.

•Mamlaka ya mapato (TRA) ni vizuri kukadiria na kutoza kodi stahiki pamoja na kukomesha swala zima la rushwa kwa maafisa wake pamoja na wafanyabiashara.

•Serikali ni vyema ikaboresha mazingira ya biashara ili kuwatambua wafanyabiashara wa jumla na rejareja, Hili litawezesha urahisi kwa kila mfanyabiashara kulipa Kodi kadri ya biashara yake ( progressive tax).

• Serikali ijenge desturi ya kutoa elimu za mara kwa mara kwa wafanyabiashara juu ya umuhimu wa kulipa kodi, na pia kutoa mrejesho wa matumizi ya Kodi inayotolewa na hao wafanyabiashara haswa kakita eneo husika.

• Serikali kupitia mamlaka zake ijielekeze zaidi kutatua kwa wakati na kwa weledi kero ambazo ulalamikiwa na wafanyabiashara, kwa kuwa kuchelewa kufanya uamuzi kunapelekea Serikali wakati mwingine kukosa mapato.
IMG-20240629-WA0035.jpg

Chanzo : Dira Makini

• Ni vizuri serikali kukaribisha wawekezaji ili kuongeza ushindani na ufanisi katika swala zima la masoko yenye mvuto kibiashara.

Mfano, Uwekezaji wa soko kubwa la kibiashara la Africa mashariki( East Africa Commercial and Logistic Center)linalojengwa ubungo stend ya zamani ya mabasi linalotarajiwa kuwa na maduka 2000 pamoja na Ofisi 200, ni muhimu miradi ya aina hiyo ikapewa kipaumbele bila kukiuka maslahi mapana ya Taifa.
IMG-20230917-WA0124.jpg

IMG-20240629-WA0034.jpg

Chanzo : EACLC (Instagram page)

Kwanini nashauri Serikali kutafuta wawekezaji?

Udadisi wangu unabaini wazi wazi Serikali kushindwa kusimamia baadhi ya masoko makubwa ya kimkakati, mfano soko la magomeni, machinga complex na maeneo mengine, ndiyo maana nashauri upatikanaji wa wawekezaji kwa sababu uzoefu unatuonesha wazi, ubunifu na tija nyingine ambazo upatikana kwenye miradi inayosimamiwa na wawekezaji.

Ambapo wamekuwa na uwezo zaidi wa kuwajibika ipasavyo kuendesha na kusimamia swala zima la biashara. Hatua naitabilia kusaidia kutanua wigo wa biashara pamoja na mapato kwa serikali na pia kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania hususani kipindi hiki ambacho upatikanaji wa ajira ni suala mtambuka katika maeneo mengi.

Kwa mazingira yaliyopo na kasi ya kidunia bila Serikali kujielekeza za kufanya uwekezaji kutumia sekta binafsi kutanua wigo wa masoko Serikali itaendelea kupata changamoto katika upande wa masoko na kiuchumi hasa kuwa kulitegemea soko moja kubwa ambalo ni Kariakoo.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom