kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Ili kuyafafanua masilahi ya Zanzibar ndani ya Muungano lazima kwanza useme kweli tupu ni kwanini Tanganyika haipo Tanzania lakini Zanzibar ipo Tanzania. Pili, useme kweli tupu kama Zanzibar ni sehemu ya Tanzania ama ni nchi. Katiba lazima inyooshe kuhusu maswali haya maana ndiyo yatakayotumika kwenye hata mgawanyo wa majukumu na masilahi ya Zanzibar na Tanganyika ndani ya Muungano.
Kama Zanzibar ni nchi ndani ya Muungano basi Katiba lazima iirudishe Tanganyika kwanza kabla ya kunyoosha maslahi ya Zanzibar kikamilifu. Na kama Zanzibar ni sehemu tu ya Tanzania basi lazima nchi ya Zanzibar iondoke ndani ya Tanzania, maana Jina la Tanzania tayari limeibeba Zanzibar na Tanganyika.
Kama Zanzibar ni nchi basi maslahi yake ndani ya Muungano lazima yaende kikamilifu kama nchi mbili kwenye Muungano, lakini kama ni sehemu ya Tanzania basi masilahi yake lazima yafuate uwiano wa mahitaji, uhitaji na idadi ya watu walioko Zanzibar. Yaani, tuseme Zanzibar, Tanga, Mwanza, Dodoma nk.
Kama Zanzibar ni nchi basi mtu kutoka Zanzibar hawezi kuwa Rais Tanganyika, Zanzibar na Tanzania na mambo yake yote kwa wakati mmoja kama ilivyo kwa mtu kutoka Bara asivyoweza kuwa Rais wa Tanzania na Zanzibar na mambo yao yote kwa wakati mmoja. Yaani Rais Mtanganyika kuna mambo hayaguzi Zanzibar, inatakiwa iwe hivyo hivyo pia Rais Mzanzibar awe na mambo ya Tanganyika yasiyo ya Muungano asiyaguse pia.
Wenzetu CCM hasa bara inaonekana hamna jicho la moyoni la kuona kisichoonekana leo kinachokuja kesho. Mnatizima ya leo kila siku hamuoni ya kesho. Afadhali kidogo CCM Zanzibar Wana muono wa mbali sana na taifa lao ndani ya Muungano na matokeo yake Leo hii ni dhahiri.
Ushauri wangu kwa maoni yangu, jambo la kwanza Kutimiza sambamba na mambo mengine ni unyooshaji wa Katiba haraka iwezekavyo ili kuondosha kero za Muungano.