Tuisheni hadi Chuo Kikuu?

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Kuna jamaa yangu anasoma UDSM mwaka wa pili, leo kanishangaza kwa kuniambia kwamba kuna baadhi ya wahadhiri wa chuo hicho, wakiwemo maprofesa, ambao husomesha tuisheni kwa baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho.

Habari hizi zimenishtua sana kwani sikutegemea wanafunzi wa chuo kikuu kusomeshwa tuisheni. Wadau mliopo hapo Mlimani naomba mtuhabarishe hii inakuwaje. Je, tuisheni inafanyika hadharani au mafichoni? Kazi ya mhadhiri ni kuelekeza--sio kufundisha. Ikiwa mwanafunzi hajaelewa mafundisho ya Profesa ni juu yake kujisomea au kujitafutia maarifa mwenyewe. Tuition & Spoon Feeding Syndrome itaiua elimu yetu.

Hii tuisheni ktk Chuo Kikuu ni dalili ya anguko la elimu yetu. Na hawa wanafunzi ndiyo lile zao la wanafunzi waliojiunga sekondari za kata huku wakiwa hawajui kusoma na kuandika. Madhara ya wanasiasa kuifanya elimu yetu kichwa cha mwendawazimu ndiyo yaliyotufikisha hapa na bado tutaendelea kushuhudia madudu mengi tu siku zijazo.

Je, nini kifanyike kurudisha elimu yetu kwenye reli?

Nawasilisha.

:israel:
 
Ni shidaaaa! Tunahitaji viongozi watakao anza kurekebisha mifumo! Then ndo wawashughulikie watendaji wa mifumo. Bila kufanya mabadiliko muhimu kwenye mifumo tutapiga marktime hapo hapo!
 
Ni shidaaaa! Tunahitaji viongozi watakao anza kurekebisha mifumo! Then ndo wawashughulikie watendaji wa mifumo. Bila kufanya mabadiliko muhimu kwenye mifumo tutapiga marktime hapo hapo!

ni kweli kabisa mkuu. elimu ilianza kuchakachuliwa tangu ngazi ya chekechea na sasa uharibifu huu umepiga hodi chuo kikuu. suluhisho ni kufumua mfumo mzima na kuusuka upya.
 
Tuisheni chuo ili iweje? Mana chuo sio swala la mitihani bali chuo ni sehemu ya kukua kimaarifa na kuona mambo katika uwanda mpana. Sasa tuition za kazi gani? Kama ni kweli hili ni janga.
 
Tuisheni chuo ili iweje? Mana chuo sio swala la mitihani bali chuo ni sehemu ya kukua kimaarifa na kuona mambo katika uwanda mpana. Sasa tuition za kazi gani? Kama ni kweli hili ni janga.

sio tu kwamba kufundisha tuisheni chuo kikuu ni suala la kushangaza, lakini pia inadhihirisha ni jinsi gani maprofesa wanaofundisha tuisheni walivyokuwa na njaa kali sana.
 
Nikiwa first year nakumbuka kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wanasoma tution changanyikeni kule...sio siri nilistaajabu,mana ukitulia mwenyewe ni vitu vinaeleweka,afu chuo muda ni mwingi sana,basi tu watu hawapo serious kusoma na wapenda kutafuniwa,
Hii tuition syndrome inakuzwa tokea utotoni naweza sema,unakuta katoto nursery tu kana tuition,jamani atacheza sa ngapi?..ukiwa in a standard school ukafatiliwa umsikilize mwalimu na ufanye homeworks lazima utafaulu vizuri naturally,mtu ambae hujasoma tuitions sekondari ushajifunza academic independence kiasi chake, kusoma tuition chuo haiwezekani..na mtu ambae all the way ni tuition hata ukiwa chuo utaihitaji tu,sijui kuna twisheni za masters,lohh elimu hii..
 
duuu hata kama sisomi chuo lakini hii imezid
 

tuition sio siri usipokuwa makini zinalemaza sana coz utategemea kila kitu tujiwa na watu km aina hiyo uwezo wao wa kufikiria na kutafakari utakuwa mdgo sana haki ya mama taifa linaangamia hili.
 
Chuo kikuu huwa kuna workshop au public lecture ambayo inatoa mwanga na mwongozo jinsi ya kurikava baadhi ya Topic,Nakumbuka kuna siku mh Membe alikuja UDOM kutoa public lecture kuhusu Tanzania Conflict resolution jinsi wanavyokabiliana nayo especially case study Malawi,chuo kikuu hakuna tution ni UKILAZA ULIOKOMAA
 

AC 100 na AC 101 hiyo ilikuwa inakimbiza wadau
 
Ndomana udom unadharaulika sasa Membe anajua nini kuhusu diplomacy hadi aje kuwapiga semina?
Yeye mwenyewe anahitaji tuisheni.

Bado hujaacha Ushoga mtoto mzuri?kitendo cha shemeji Yako kumtenda dada yako usilete hasira kwa wana UDOM wote,kisa ni Mwanafunzi wa UDOM, sasa tukiacha siasa wewe na yule nani anajua vitu zaidi ?kitendo cha Mtu kuwa katika field husika ni tofauti na wewe ulikuwa unasoma Vitabu,PDF, na research za kale.
 

Ndiyo maana bodi ya mikopo wanawapa Tuition Fee
 
Tuition zipo na watu wanalipa hela mbaya, ila majority ya wanaopiga tuition ndo' utakutana nao kwenye kusapua a.k.a semina elekezi.

maprof wanaofundisha hizo tuisheni si watakuwa na njaa kali sana?
 
Ndiyo maana bodi ya mikopo wanawapa Tuition Fee

kwa hiyo tuition fee ndio kazi yake hii kwa uelewa wako? sio kwamba inalipwa moja kwa moja chuoni? we kilaza nini?
 
kwa hiyo tuition fee ndio kazi yake hii kwa uelewa wako? sio kwamba inalipwa moja kwa moja chuoni? we kilaza nini?

Mimi si kilaza mkuu,
My undergraduate GPA at UDSM was 4.2
What's yours?
 
sio tu kwamba kufundisha tuisheni chuo kikuu ni suala la kushangaza, lakini pia inadhihirisha ni jinsi gani maprofesa wanaofundisha tuisheni walivyokuwa na njaa kali sana.

Ukisikia kuwa unatakiwa ulipe Tuition fees huwa unaelewaje? Tuanze na hapa kwanza
 

Habari zenyewe huna uhakika nazo halafu unamake conclusion unategemea nini.
Wapi kwingine umesikia kuna hiyo unaita tuisheni au ni UDSM pekee yake?
Huyo aliyekwambia hakukwambia kila kitu kilivyo?
 
Mimi si kilaza mkuu,
My undergraduate GPA at UDSM was 4.2
What's yours?

tuition fee ni ya kusomea tuisheni? hizo hela mnalipwa cash kama boom? wewe lazima utakuwa kizazi cha division 5. BTW kuwa na GPA kubwa uliyoipata kwa kukariri sio kigezo cha kuelimika au kuwa na maarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…