Tuishi upendo tunaofundishwa kwenye imani zetu ili tuwe vielelezo bora vya imani zetu

Tuishi upendo tunaofundishwa kwenye imani zetu ili tuwe vielelezo bora vya imani zetu

Half american

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
38,283
Reaction score
97,793
Lengo la dini ni kuhamasisha waumini wake kuishi maisha ya upendo na yenye nidhamu kwenye jamii. Tunafundishwa kutambua yapi ya kufanya (mema) na yapi ya kutokufanya (mabaya yenye machukizo kwetu na kwa Mwenyezi Mungu).

Inashangaza sana watu wenye utashi wa kutambua mema na mabaya wanafanya mambo ambayo ni kinyume na imani. Najua hatujakamilika kama binadamu, kuna mambo ni ngumu sana kutokufanya hata kama tunakosea, lakini kuna mambo mengine tunafanya hata shetani na uovu wake anashangaa ni nini hiki.

Unashiriki ibada kila iitwapo leo na hutaki na huna kusudio la kubadilika, huko kwenye ibada unaenda kufanya nini kama hautaki kubadilika na kuishi maisha ya upendo?

Kutwa kucha mtu upo na kukimbizana na mambo ya kiimani lakini kwenye jamii unaishi maisha ya ajabu na yenye kuwaumiza wengine bila kujali chochote mpaka watu wanajiuliza hivi huko kwenye nyumba za ibada huwa anafuata nini, au ndio anayofundishwa huko? Matendo yako yaendane na imani yako, wengi wanakuwa vielelezo vibaya kwa imani wanazoamini.

Kuna watu ni waumini wazuri sana na wanyenyekevu huko kwenye dini ila ndio vinara wa kutelekeza watoto na familia, unyanyasaji, uchonganishi, kukwepa majukumu, uchawi n.k.

Tuishi upendo tunaofundishwa kila leo kwenye imani zetu.
Jumapili njema.
 
Dini haina uwezo wa kufanya watu wawe na upendo , dini yenyewe haina hata chembe ya upendo itasababishaje watu wawe na upendo ?
Tunayohubiriwa huko ni upendo, kwa imani yangu ndio huwa nayasikia sana sijui huko kwenye imani nyingine.
 
Watu wanaoshika dini saaaana huwa baadhi wanakuwa na chuki hatari tena hata kwa wenye Imani Moja na wao
Wale moderate ndio huwa watu poa
Sijui kwanini huwa hivi? Kuna uhusiano gani kati ya kushika dini sana na kuwa muovu wa kisiri siri.
 
Kivipi? Fafanua
Kabla ya Kuenea kwa Ukristo na uislamu Watu waliishi kwa amani japo ilikuwa sio Amani kubwa ila ilitosha..
Ila baada ya Dini kuingia Chuki imekuwepo Vita nyingi ni kwa sababu ya Dini..

Na hata Sisi kwa sisi Tunaochukuliana Waasi, Wenye dhambi na kudharauliana kujipa Umuhimu usiofaa kwa wengine na kudharau wengine kujiona bora kuliko mwingine..

Leo hii Mchungaji au Sheikh anaonekana ana thamani kuliko Muuza Gongo kwa sababu tuna imaginary cleansheet ya Kuishi na u"saint" tuliyojiwekea Wenyewe kwamba Kipi ni haki na Kipi sio haki na kipi ni dhambi na kipi sio dhambi..

Watu wanaofanya kinyume na Vitabu Vyetu vinavyosema Tunawaona maadui na Mostlty tunawaita majina mabaya kwa sababu tunaamini sisi tu wateuliwa..

Huu ndo upendo unaozungumzia???
 
Back
Top Bottom