Anita Baby
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 1,265
- 540
Niondoleeni ukusi ukusi wa mawazo. Fasihi simuliz iliyoandkwa 2iteje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niondoleeni ukusi ukusi wa mawazo. Fasihi simuliz iliyoandkwa 2iteje?
kwa mtazamo wangu,inabakia kuwa fasihi simulizi sema tu imehifadhiwa katika maandishi ili isipotee..
Niondoleeni ukusi ukusi wa mawazo. Fasihi simuliz iliyoandkwa 2iteje?
Inaitwa Fasihi andishi
Hii ni sanaa itumiayo maandishi kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
Fasihi andishi hugawanyika katika matawi mawili: nathari na ushairi.
Pia fasihi andishi ina tanzu nyingi mbalimbali, hasa riwaya, tamthiliya, insha, shairi n.k.
Kulingana na mada ya kazi ya kifasihi, inawezekana kutofautisha bunilizi na kazi zinazowakilisha ukweli.
Marejeo: Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.
sio sawa kusema kuwa ni fasihi andishi, kwani uwasilishwaji sio kigezo pekee cha kuitambua fasihi. ile ni fasihi simulizi iliyohifadhiwa kwenye maandiko.
uko sawa, kwa kuwa ishu sio kuandikwa, ishu ni msingi wayo. Hata nyimbo ni fasihi andishi ingawa huimbwa mdomoni.