Tuiulize serikali maswali muhimu, ambayo inatakiwa kutoa majibu sahihi

Background Check

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2019
Posts
341
Reaction score
498
Kwa mawazo yangu ya kawaida bila kutumia akili za shuleni kwetu kuna vitu havipo sawa kwenye chi hii.

Mfano: Unaenda RITA unafanya maombi ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto/watoto etc.. unapewa control number unalipia baada ya muda unafata cheti chako kipo tayari.

Cheti kipo tayari kwa matumizi, unaenda kwenye ofisi nyingine ya serikali mfano NHIF kufanya utaratibu upate bima, cha ajabu kabisa unarudishwa RITA (ulipotoka). Unaambiwa uende ukaverify cheti hicho akigonge mhuri huyo RITA.

Unafika RITA kuverfy hicho cheti ambacho ametoka kukupa huyohuyo RITA, Ajabu RITA huyu anakwambia tena umpe 6000 ili athibitishe hicho cheti.

Kama kilitakiwa kiwe na mhuri, kwa nini RITA asikigonge mhri kabisa?

Serikali na watendaji wake kila mmoja kwa nafasi yake hili halipo sawa hata kidogo.

Waziri Dkt. Gwajima D
Na mawaziri wengine wenye dhamana.
Msaidieni Rais kwenye mambo kama haya.

Ondoa Ukiritimba.
 
Mianya ya usumbufu na kula pesa za wanyonge
Yale yale ya Mahakamani, umeshinda kesi alafu bado unaambiwa kafunguwe kesi nyingine ya kukazia hukumu, hapo unakua kama mnaanza tena moja kuungurumisha kesi, maana na upande wa pili wanakuja na mapingamizi yao kwenye kesi ya kukazia hukumu! Ni kind of kama kautapeli flani hivi kwa wanasheria!!
 
Haya na mengine mengi yanatakiwa kuwa sababu kuu ya kuifurusha serikali ya mama wa kizimkazi!
Kwamba serikali itakayokuja baada ya mama kizimkazi itatatua tatizo hilo?
 
Tunataka serikali inayowajibika kwa watu,ya samia imeshindwa kuwajibika kwa raia badala yake inawaua kubalance daftari la wapiga kura
Kwamba serikali itakayokuja baada ya mama kizimkazi itatatua tatizo hilo?
 
Bi kidawa umemuuliza? Anasemaje?
Bila shaka una maanisha Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Nadhani inapendeza ukimpa heshima yake aliyopewa na katiba.

Nimeleta maada ili wahusika waone na walifanyie kazi hili, yeyote katika nafasi ya maamuzi, iwe Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri wenye dhamana ama viongozi waandamizi ngazi za kutoa maamzi juu ya hili.

Sahihi yangu
Machepele wa Tanzania
 
Mianya ya usumbufu na kula pesa za wanyonge
Watuonee huruma hawa watu.
Tuna lipa kodi kila sehemu Mandatory TAX, Pay as you earn, Bima ya afya, Lesen ya biashara, service Levy, 18%, withholding tax, etc...
 
Yale yale ya Mahakamani, umeshinda kesi alafu bado unaambiwa kafunguwe kesi nyingine ya kukazia hukumu, hapo unakua kama mnaanza tena moja kuungurumisha kesi, maana na upande wa pili wanakuja na mapingamizi yao kwenye kesi ya kukazia hukumu! Ni kind of kama kautapeli flani hivi kwa wanasheria!!
Yaaaniii file movement nauli na mafuta hapo kibao utajutaaa
 
Mianya ya usumbufu na kula pesa za wanyonge
Tunatakiwa tuungane kuiambia serikali isikilize kutokea chini na siyo juu.

Ni wazi, ikiwa wanasiasa wanaamini kwamba wapiga kura hawawezi kuaminiwa na ukweli, demokrasia iko hatarini sana. Ili demokrasia ifanye kazi ni muhimu kwamba serikali iheshimu watu na kuwachukulia kwa uzito, sio tu wale ambao wameipigia kura serikali hiyo, bali watu wote. Zaidi ya hayo, ili kutumia haki zao za kidemokrasia ipasavyo, watu wanapaswa kufahamishwa kikamilifu iwezekanavyo.

Sahihi yangu
Machepele wa Tanzania
 
Kwa mawazo yangu ya kawaida bila kutumia akili za shuleni kwetu kuna vitu havipo sawa kwenye chi hii.

Mfano: Unaenda RITA unafanya maombi ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto/watoto etc.. unapewa control number unalipia baada ya muda unafata cheti chako kipo tayari.

Cheti kipo tayari kwa matumizi, unaenda kwenye ofisi nyingine ya serikali mfano NHIF kufanya utaratibu upate bima, cha ajabu kabisa unarudishwa RITA (ulipotoka). Unaambiwa uende ukaverify cheti hicho akigonge mhuri huyo RITA.

Unafika RITA kuverfy hicho cheti ambacho ametoka kukupa huyohuyo RITA, Ajabu RITA huyu anakwambia tena umpe 6000 ili athibitishe hicho cheti.

Kama kilitakiwa kiwe na mhuri, kwa nini RITA asikigonge mhri kabisa?

Serikali na watendaji wake kila mmoja kwa nafasi yake hili halipo sawa hata kidogo.

Waziri Dkt. Gwajima D
Na mawaziri wengine wenye dhamana.
Msaidieni Rais kwenye mambo kama haya.

Ondoa Ukiritimba.
Hii nchi kuna upumbavu wa hali ya juu sana.
 
Yale yale ya Mahakamani, umeshinda kesi alafu bado unaambiwa kafunguwe kesi nyingine ya kukazia hukumu, hapo unakua kama mnaanza tena moja kuungurumisha kesi, maana na upande wa pili wanakuja na mapingamizi yao kwenye kesi ya kukazia hukumu! Ni kind of kama kautapeli flani hivi kwa wanasheria!!
Kuna kanuni maarufu iitwayo 'LAMESIA ANGLIKANA iliyobadilikia nchini Tanzania na kuwa LAMESIA TANGANYIKANA' Yaani ni heri wenye haki hamsini wafungwe gerezani kuliko mtuhumiwa mmoja kuranda huru mitaani. Hii ni kinyume na ile LAMESIA ANGLIKANA inayosema ni heri waasi 50 waende wakafungwe gerezani kuliko mwenye haki mmoja kufungwa gerezani.

Chapa yangu ni
Machepele wa Tanzania
 
Haya na mengine mengi yanatakiwa kuwa sababu kuu ya kuifurusha serikali ya mama wa kizimkazi!
Ni wazi, ikiwa wanasiasa wanaamini kwamba wapiga kura hawawezi kuaminiwa na ukweli, demokrasia iko hatarini sana. Ili demokrasia ifanye kazi ni muhimu kwamba serikali iheshimu watu na kuwachukulia kwa uzito, sio tu wale ambao wameipigia kura serikali hiyo, bali watu wote. Zaidi ya hayo, ili kutumia haki zao za kidemokrasia ipasavyo, watu wanapaswa kufahamishwa kikamilifu iwezekanavyo.

Chapa yangu
Machepele wa Tanzania
 
Back
Top Bottom