Tujadili Kiukweli (Wanaume tu)

Kaka nadhani ni 'apetite' imekubana wala si kingine...kwa maelezo yako inaonekana hii tabia ya mkeo hakujifunzia kwako (chunguza kwao) ila kwa sababu ya upeke peke 'wetu' wa kiume ukafumba macho...sasa maid wako kang'aa mguu huku akitimiza wajibu roho inataka kukutoka lol! Nikicopy bila kuedit ushauri wa V. of Reason "...ukiona kama ni kero sana basi tafuta Houseboy.
Ukigusa hapo huenda hata hiyo heshima unayopata sasa ikaisha wewe ndio ukaishia kuwanawisha wote mikono na kufua nguo"
 
kula zigo hilo... Halafu hujatueleza kama hg mzuri au vipi??

Kila la kheri kwenye kushiriki dhambi na kuvunja amri ya sita braza

badae
 
Wanawake wengi huwa hawawaelewi wanaume. Wanadhani kama una-do basi inatosha.
 

Lakini wanaume nao akiamua kutokua mwaminifu, huwa wanatafuta kisingizio chenye nguvu ambacho watu watakielewa, ili badae ajidai nilifanya hivi kwa ajili ya hivi hata kama si kweli.
 
Lakini wanaume nao akiamua kutokua mwaminifu, huwa wanatafuta kisingizio chenye nguvu ambacho watu watakielewa, ili badae ajidai nilifanya hivi kwa ajili ya hivi hata kama si kweli.
angalau huyu ameomba msaada,ujue amechoshwa na hizo tabia,na ame admit alichotaka kufanya kwa HG lakini hakukifanya.hiyo ni mifano tosha kuwa s.times na wao wanachoshwa na tabia ambazo wao hawazipendi kwa wake zao.na w.ume sio sana kulalamika nje,mpaka amelalamika humu,ujue hicho kitendo kimeshamchosha
 
Nikweli unayosema, yote yanawezekana. Ila saingine na wake za watu hua wanajisahau, tena bahati huyo ni HG. Mh ngoja akutane na wadada wanao maanisha, akiingia tu kwako karibu, pole na kazi na foleni unakunywa nini, pumzika mzee anapewa na the guardian asome kidogo na mambo kibao mbona huyo mama atajua kumpokea mzee wake. Hajaibiwa bado, uvivu utageuka chapakazi, naona hajakutana na mi nguri.
 


kiongozi umeongea jambo la msingi kabisa,
Mwenye macho haambiwi tazama,

NARUDI, NGOJA NINYWE MAJI KWANZA!!!!LOL....
 
huyu mama ni uvivu tu ndo unamsumbua. na wa dizaini hii wapo wengi kusema kweli.
jaribu kumwelewesha mambo anayotakiwa kukufanyia na sio hg.akishindwa aende kwao basi akapumzike vizuri halafu akijiona nguvu za kufanya hayo mambo zipo basi arejee mwenyewe.

na lingine ukute ni mjamzito kwa sasa hivi ila hajajitambua,maana mimba nyingine zinaleta na uzembe mwilini hajisikii kufanya lolote.
 

Kijana juzi,

Nianze kwa kukuomba radhi kwani nitakwambia ukweli kuwa tatizo la mkeo ni wewe mwenyewe na suluhisho ni wewe mwenyewe.Unachotakiwa kufanya ni kukaa naye na kumweleza ukweli tena si kwa jazba ila tafuta muda wakati akiwa ktk hali ya raha yaani good mood,umweleze nini usichokipenda na nini unapenda katika ndoa yenu. Hakuna binadamu anayependa kulaumiwa au kugombezwa, ndo maana nimenza na kukuomba radhi,Vivyo hivyo fanya kwa mkeo.Atakapogundua kuwa alikuwa anakosea atakuona wewe ni shujaa.

Wengi wengi tunafikiri kuwa suluhisho la matatizo yetu ya ndani ni watu wengine au hadhara ya watu.Siajabu mkeo hajuai kama wewe unachukia kwa yeye kutokupokea mizigo unaporejea kazini.

Nikuulize, Je, wewe ulishawahi kumpokea mizigo akitoka kazini?

Je,Ulishawahi kuandaa chai na kuwita mnywe hata siku moja................????

Mwisho, Mshukuru sana Mungu kukupa mke,nikupongeze hapo kwenye blue mpende na mthamini sana,isitoshe anakupenda na wewe mwenyewe umekiri. Ni mama Mtoto wako huyo

Kaza buti kaka..............
 
kula zigo hilo... Halafu hujatueleza kama hg mzuri au vipi??

Kila la kheri kwenye kushiriki dhambi na kuvunja amri ya sita braza

badae

kwan akiwa mbaya itagoma?
uzuri ninin na ubaya ninin?
 
Huyo atakuletea uvivu mpaka kitandani..anza kuchakachua hg mapema! halafu pia umpige sopsop la nguvu apendeze kinyama kila anapopita ananukia tu mtoto anawaka! Halafu uone kama atapewa nafasi ya kukunawisha tena
 
Huyo atakuletea uvivu mpaka kitandani..anza kuchakachua hg mapema! halafu pia umpige sopsop la nguvu apendeze kinyama kila anapopita ananukia tu mtoto anawaka! Halafu uone kama atapewa nafasi ya kukunawisha tena

Akifanya hivyo ipo siku atarudi kutoka kazini akute HG kapandishwa basi la jioni kurudishwa kwao Maneromango! Poor her!
 
Anaza Ndoa Viktim....

Afu acha kujibaraguza... ungemlamba ungekuja kusema hapa? Tutajuaje kama umebanjua kweli maana nyie ndo wale mnatoka job saa 4 kuvizia HG's....

Hivi kwanza kazi ya kuhudumia watoto, kupika, kufua, kusafisha nyumba ni ya mwanamke tu? Je kama huyo mwanamke anaenda kazini kama wewe na mnarudi muda sawa?

Halafu kweli we dikteta, hata kiatu chako kupiga kiwi unashindwa hadi afanye mkeo? Nyie ndo wake zenu mnawageuza watumwa na sio wasaidizi
 
Swali Tafadhali wandugu,

I might be going out of topic though, Ni kosa sana kwa msichana wa kazi kuingia chumbani kwa baba ma mama? mbona wengi wetu wenye hizi nyumba tunazoita double room wasichana wanaingia na kutoka tu?
 
kaaaaaaazi kweli kweli, afanyacho mkeo si kizuri ila unashindwa hata kupiga kiwi kiatu chako baba? kuna kazi zingine inabidi na nyinyi wababa mjizoeshe kufanya wenyewe hata kusafisha bafuni kwenu, siku nyingine unamfulia chupi mkeo. Nasema hivi kwa sababu siku mkeo (kwa sababu ni mfanyakazi) amesafiri kikazi au masomoni, ni nani atakefua chupi zako na kusafisha bafu/choo chenu baba na mama? ni nani atakaekupigia kiwi n.k sishabikii kwamba mama asikufanyie, mama ni wajibu wake kufanya ila na wewe baba jitahidi tahidi ili siku mkeo akiwa hayupo usipate tabu mtanisamehe nimeingilia uwanja wa wababa
 

wee umeambiwa ni kwa wanaume tuu?? are yu a man??shame on yu wewe sasa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…