Wao ni zuri, lakini taifa limechakachukuliwa kwani kwenye kuundwa kwa ille tume ya akina Prof Maboko watanzania walitangaziwa kuwa tume imeundwa, lakini kwa uzembe wa hali ya juu sidhani kama hao Watanzania walitangaziwa kuhusu majibu ya ile tiume so tunaweza kusema kwamba Makenya Maboko amegalagaza heshima yake kama wakati ule alipopewa ile tume ya Baraza la mitihani.
Na sidhani kama kuna mtanzania yeyote asiyejua matatizo ya hii bodi ya mikopo na kwa mda mwingine huwa nakaa na kuwaza kuwa huwa serikali yetu haielewi hata maana ya kumkopesha mtu. Na endapo wakiendelea na ule utaratibu wao ni vyema tufanye mpango wa kuifanyia hii bodi Nomeclature mpya kwani haina maana yeyeote ya kuiita bodi ya mikopo huku walalahoi wa kitanzania hawapati huo mkopo ambao wataurudisha ipasavyo.
MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU IBARIKI BODI YA MIKOPO.