Tujadili kwa maslai ya nchi: Magufuli anasema makampuni makubwa ya madini yamezalisha dhahabu ya sh. tril. 2.2 na nchi ikaambulia bil. 68

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Naonba niwe muwazi kwa nchi kama wawekezaji wanachimba dhahabu ya shs. tril. 2.2 kwa mwaka huu na nchi kupata bil. 68 pekee ni aibu.

Kwa analysis hiyo naona wachimbaji wadogo wanachangia pakubwa kuliko hao wachimbaji wakubwa na tunasema Sheria ya Madini tunapata 50% kwa 50% kwanini wanatudanganya?
 
We endelea kumsikiliza Zitto na madai yake uchwara serikari imepoteza $30 billion kwenye Gas investment.

Mnachukulia haya mambo poa sana as if hiyo hela inatolewa kama sandakalawe tu.

Hawa jamaa wanachovuna na ukiona hizo hesabu zao hadi upate chako ni kama umegawa tu mali zako ukiingia kichwa kichwa, ndio kinachowakuta huko kwenye madini.
 
Siamini hii kitu, haiwezekani wachimbaji wadogo wakachangia zaidi ya wawekezaji wa nje, hapo tumedanganywa, lakini kama ni kweli hiyo yote imechangiwa na serikali ya CCM, wazee wa 10% mikataba inasainiwa hotelini ulaya.
 
Malumumba utasikia sasa madini safi!Shwain,wamshukuru zitto maana alipambana sana walau ikaongezeka!Kipindi hicho miCCM akiwemo Magufuli walimfukuza bungeni kwa hoja yake ya madini!
 
Wewe hata hujui mambo ya madini tulia,
Hicho alichosema ni mrahaba.
Sasa toafautisha mrahaba na faida ya nusu kwa nusu ambayo inatoka na hisa,

Mbona mnajifanya vipofu na viziwi?
Hata huna asante kama kabla ya kubadilisha mikataba tulipata bilioni 50 na sasa ni mara mbili bado ti huoni ni jitihada?

Kumbuka hiyo mikataba kama unaona bado ni ndogo basi mgombea wenu alisema kwa kiwango hicho tulifukuza wawekezaji sasa ina maana yeye angepunguza hizo kodi.
 
Nyumbu katika ubora wao!
 
Kusikiliza na kuelewa ni vitu viwili tofauti ,umesikia hujaelewa
 
hizi data umezitoa wapi? magu hajasema hivyo usimlishe maneno
 
Kumbe serikali ya John bado inawanufaisha mabeberu kupitia madini. Tumeambulia bil. 68 tu kati ya tril.2.2?
 
Kwani hujui hii awamu inaongozwa na mtu muongo na mpika data feki duniani
 
Sidhani hata umemuelewa,

Serikali haina faida ya 50 kwa makampuni yote hiyo ilikuwa deal na Barick tu.

Alichozungumzia Rais ni Royalty(mrabaha).
 
Forgetful lier himself,hiyo 50% kwa 50% ni siasa.Tangia mwanzo CCM hawana jambo lolote wanaloweza kufanikisha,Failure after failure.Hizo takwimu haziakisi kuwa sekta inainufaisha nchi.
 
Siamini hii kitu, haiwezekani wachimbaji wadogo wakachangia zaidi ya wawekezaji wa nje, hapo tumedanganywa, lakini kama ni kweli hiyo yote imechangiwa na serikali ya CCM, wazee wa 10% mikataba inasainiwa hotelini ulaya.
Halafu inawekwa SIRI hata kwa Bunge letu,huu ni wizi kama wizi mwingine.Haya ndiyo mambo yanayoenda kupatiwa ufumbuzi baada ya CDM kuingia madarakani October 2020.Watanzania tusipoiondoa CCM tutaendelea kuwa na hali mbaya zaidi.
 

Kesho watabadili.

Na hiyo hotuba ya leo hutoiona wala kuisikia popote.

Kesho watasema Serikali ilipata 568 bilion.

Tega sikio utamsikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…