DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Ibara ya 19(b) ya Katiba ya CCM ya 1977, Toleo la 2022 inatoa fursa ya Kiongozi KUJIUZULU.
UTARATIBU
Makamu Mwenyekiti CCM anapojiuzulu hutakiwa kukabidhi barua ya kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa chama Taifa. Kisha, Mwenyekiti anatakiwa Kikatiba (CCM) kuipeleka kwenye Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. Hiki ndicho chombo chenye mamlaka ya KURIDHIA au KUKATAA kuridhia kujiuzulu kwa huyo kiongozi.
Kama chombo hiki kitaridhia, rais au Halmashauri Kuu itatakiwa kuitisha Mkutano Mkuu wa chama Taifa kwa ajili ya uchaguzi huku ikipeleka jina la Kada aliyeteuliwa ili apigiwe kura awe Makamu Mwenyekiti mpya wa chama.
Siku ya Mkutano Mkuu (ambao huwa wazi), Mwenyekiti wa Chama Taifa atasoma hadharani barua ya KUJIUZULU huko, tena mbele ya Vyombo vya Habari aliyoipokea toka kwa Makamu wake. Mfano wa hili ilifanyika tarehe 1 April 2022, ambapo Mwenyekiti wa CCM (SSH) alisoma barua ya kung'atuka toka kwa mzee Philip Mangula.
Kwakuwa Mwenyekiti wa CCM sio MAMLAKA ya Uteuzi ya Makamu wake, kuridhia kwake (rais) hakuna nguvu ya kisheria au Katiba ya Chama. Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ndiyo yenye mamlaka hayo. Hivyo, kama Halmashauri Kuu haijaridhia mzee Kinana KUJIUZULU, basi Katiba ya CCM bado inamtambua mzee Kinana kama Makamu Mwenyekiti (Bara).
Jambo ambalo binafsi nalisubiri ni kuona kama Mwenyekiti wa CCM Taifa ataisoma barua hiyo anayosema amepokea ya mzee Kinana mbele ya Mkutano Mkuu.
Ukitaka kuelewa haya niliyoyasema, nenda pitia Katiba ya CCM Ibara 19(b) & (e), sambamba na Kanuni za Uchaguzi CCM 116(d) toleo 2017.
Pia, Ibara za 105 & 106 za Kanuni za Uchaguzi za CCM, sambamba na Katiba CCM ibara 100(5)(a) & 114(1), toleo 2020.
Malizia na Ibara ya 102(12)(a) ya Katiba CCM, pamoja na Kanuni za Uchaguzi za CCM, Ibara ya 106.
Kama kuna lolote la ziada, nitafurahi kujifunza..
Je, mzee Kinana AMEJIUZULU au AMEFUKUZWA, nimeshawafungua macho kwenye hili.
karibuni Tujadili.
Pia soma
- Kuelekea 2025 - Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia