TUJADILI: Logic ya CCM kuhalalisha serikali mbili waliitoa wapi?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Habari wadau,

Mimi naomba kuuliza hivi hawa wana -CCM wanapata wapi kiburi na uhalali wa kusema serikali mbili ndio mfumo sahihi na unaoukabilika na watanzania wengi?

Labda niullize ni lini watanzania waliwahi kupewa fursa ya kupiga kura ya maoni juu ya muundo wa muungano na kuridhia muundo wa serikali mbili?

Wakati mwingine huo najiuliza,hivi ni kipi kilipaswa kuanza,mchakato wa kuandika katiba mpya au kura ya maoni kuamua hatima ya muungano na muundo wa muungano wenyewe?Hapa ni kipi kilipaswa kutangulia kati ya haya mambo mawili?

Mimi naamini hata tukipata katiba mpya,ipo siku tutarudi kupiga kura kuamua hatima ya huu muungano,

Kura ya maoni juu ya hatima na muundo wa muungano ni "deni" kwa watawala na ipo siku watalazimika kulilipa?

Nawaonya watawala hili "deni" halikwepeki bali riba(interest) ya deni hili inazidi ku-accumlate siku hadi siku.
 

CCM bana wanamuenzi Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika suala hilo, Ila yafuatayo waliona hayana haja ya kuendelea kumuenzi Mwalimu,
1. Azimio la Arusha na Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea,
2. Viongozi kuwa na hisa katika makampuni
3. Viongozi kumiliki biashara ukiwa katika utumishi wa UMMA
4. Kukabidhi raslimali za Taifa kwa wageni na kwamba wazawa wao wauze juize na soda tu
5. Kuhakikisha Meno ya tembo yanaendelea kupelekwa ughaibuni
6. Kutibiwa nje ya nchi
7. Kuua Elimu kabisa na kuongez Divisheni V
8. Gesi itoleweMtwara iende Dsm
9. Zidumu fikra za Mwenyekiti
 
Hata kama ingelikubalika mfumo wa serikali mbili ndilo chaguo la watanzania walio wengi, bado kuna hoja ya kwamba serikali ya CCM imeshindwa kabisa kulinda mfumo huo; hii inatokana na ukweli kwamba marekebisho yaliyofanyika kwa katiba ya Zanzibar katika miaka ya hivi karibuni siyo tu yanavunja katiba ya muungana wa Tanzania bali pia yameifanya Zanzibar kuwa kama nchi inayojitegemea. Ukweli huu ndio uliofanya Tume ya katiba ifikie uamuzi kwamba hapakuwepo na njia nyingine ya kutatua tatizo hilo bali mfumo wa serikali tatu.
 
Serikali TATU (3) ndio suluhisho la kero za mungano zilizokuwa hazitatuki na zilizokuwa zimedumu miaka 50 ila chama chetu ni waoga kwa hilo na wanapower ya kuwasemea wananchi mawazo yao
 
...Kura ya maoni juu ya hatima na muundo wa muungano ni "deni" kwa watawala na ipo siku watalazimika kulilipa?

Nawaonya watawala hili "deni" halikwepeki bali riba(interest) ya deni hili inazidi ku-accumlate siku hadi siku.
Binafsi nakubaliana na hoja ya serikali mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar. Hiyo ya muungano tuwaachie Mwl Nyerere na mwenzie Karume. Lau kama kweli tunataka kuungana, basi na iwepo serikali moja tu!
 
Binafsi nakubaliana na hoja ya serikali mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar. Hiyo ya muungano tuwaachie Mwl Nyerere na mwenzie Karume. Lau kama kweli tunataka kuungana, basi na iwepo serikali moja tu!


Ule muungano uliofanywa na Nyerere na Karume ulikidhi mazingiara ya cold war ya wakati ule; hivi sasa kama kweli tunataka MUUNGANO basi ni lazima tuwe na serikali moja!! Haiwezekani nchi bili huru zikaungana halafu mkawa na serikali TATU huo ni unafiki. Aidha mnaungana kikweli kweli na kuwa wamoja au kila nchi inakuwa na serikali yake nikiwa na maana kuuvunja MUUNGANO kama ulivyo sasa bila kuwa wanafiki!!
 
Binafsi nakubaliana na hoja ya serikali mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar. Hiyo ya muungano tuwaachie Mwl Nyerere na mwenzie Karume. Lau kama kweli tunataka kuungana, basi na iwepo serikali moja tu!

Makofi tafadharii!
 
Reactions: SMU
Yalikuwa mawazo tu ya baba wa taifa. Marehem Karume hakuwa na wazo hilo.
 

Wanaogopa mageuzi ambayo haryana uhakika wa hatma yao binafsi.
 
Binafsi nakubaliana na hoja ya serikali mbili, yaani Tanganyika na Zanzibar. Hiyo ya muungano tuwaachie Mwl Nyerere na mwenzie Karume. Lau kama kweli tunataka kuungana, basi na iwepo serikali moja tu!

Na mimi naunga mkono muundo wa serikali zote: tatu yaani Tanganyika, Zanzibar na SJMT, Mbili yaani Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar( hapa muundo huu wa mbili za sasa siuafiki). Mwisho na mfumo halali wa Muungano ni Serikali 1!
 
Reactions: SMU
Wanaogopa mageuzi ambayo haryana uhakika wa hatma yao binafsi.
Kimsingi mageuzi hayaepukiki, ingawa yanaweza kuchelewa. Ndicho Mhe. Jaji Warioba alichowaambia Watanzania na wana CCM, kwamba iwapo tutafumbia macho suala la serikali tatu basi litakuja kwa nguvu tukiwa tushachelewa kufanya maamuzi.
 
Duh mimi ni tofauti tukirudi na serikali tatu lazima turudi kwenye azimio la arusha ambalo lilivunjwa na azimio la zanzibar kama wadau mnakumbuka sasa kulirudisha azimio sijui litafanyika wapi, na hawa ndugu zetu tukiwa na serikali tatu mamlaka ya tanganyika yatawaangalia watanganyika kwa karibu zaidi na wao wameishawekeza sana tofauti na watanganyika sana sana mtanganyika amewekeza kwenye ndoa huko znz, na kwa nini jumuiya ya afrika mashariki ni nchi 5 kwa hiyo tukiwa na serikali tatu znz itabidi iombe kujiunga na jumuiya ya afrika mashariki, kwa hiyo tutakuwa na jumla ya wanachama 7 yaani tanzania, tanganyika, znz, kenya, uganda, rwanda, burundi. Ni mtazamo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…