EllySkyWilly
JF-Expert Member
- Aug 28, 2020
- 2,204
- 2,085
Habari za leo wakuu,
Uzii huu utakuwa maalum kuijadili sera yetu ya viwanda.
Bila kutukana wala kumnyoshea mtu yeyote kidole, naomba kila mmoja atoe maoni yake.
Mada: Wewe unahisi sera yetu ya viwanda ina mapungufu gani?
Zingatia ili taifa letu liweze kuendelea linahitaji kuwa na sera bora ya viwanda. Sera bora ya viwanda inatakiwa kutoa dira ya maendeleo ya uchumi wa taifa.
Zingatia muda mwingine sera inaweza kuchukua mda mrefu kuleta matokeo chanya.
Sote tumeona jitihada zinazo fanywa na serikali yetu ya awamu ya tano na sita katika kutoa motisha kwa watanzania kujenga na kuanzisha viwanda.
Lakini pia tumeona jinsi ambavyo serikali imetumia jitihada kufufua taasisi za umma. Serikali imefufua ATCL, TTCL, n. k.
Zingatia mfumo wowote wa biashara ya kiuchumi hauwezi kufanya kazi vizuri bila serikali kuingilia. Hivyo ni lazima serikali nayo iingie kwenye mfumo huo ili kazi iende vizuri. Ndio sababu mnaona kwenye usafiri wa anga mnaiona serikali kupitia ATCL, kwenye mawasiliano mnaiona serikali kupitia TTCL, n.k.
Serikali ikiwa karibu na mfumo wa kiuchumi ni rahisi kupata taarifa zinazo husu mzunguko mzima wa kiuchumi, kasoro na matatizo mbalimbali. Mimi nadhani pia kuiachia sekta binafsi iendeshe mfumo mzima wa uchumi peke yake sio vizuri na swala hili lina athari kiuchumi.
Nikija kwenye swala la mchakato mzima wa sera yetu ya viwanda. Sera yetu ni nzuri sana na itatuletea faida nyingi sana huko mbeleni. Ila nilikua napenda ili sera yetu ifanikiwe asilimia 100 hasa kwenye swala la ujenzi wa viwanda, nadhani ingechagua baadhi ya viwanda vile ambavyo tunaona tunaweza kuviendesha vizuri na vikatatuletea faida nyingi kama vile utoaji wa ajira nyingi, mapato mengi na bidhaa nyingi.
Nilikua nasoma jarida moja jinsi ambavyo china wanapigana kukuza uchumi wao, wao katika sera yao ya viwanda wamechagua utengenezaji wa magari ya umeme. Hivyo nguvu yao yote wameilekeza kwenye uwekezaji wa viwanda vya magari ya umeme, utafiti na ubunifu katika viwanda vya magari ya umeme.
Naomba niishie hapa.
Hivyo ndugu yangu kama una maoni dondosha maoni yako
Usitukane.
Hiki ni moja ya kiwanda katika Tanzania yetu ya viwanda.