Tujadili nyumba wanazojengewa Marais Wastaafu Tanzania

Umeeleweka vizuri

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Siasa ni Sayansi
 
Ben alimjengeaga JkN kule Mwitongo kwa kuwa aliona hakuwa na nyumba ya hadhi ila hawa wazee ambao walikula hela zetu mabilion kwa mabilion siungi mkono

Marais WOTE wana MAHEKALU YAO TAYARI,

HII MAMBO Magufuli UMETOA WAPI?

YANINI?

KWA FAIDA GANI?

Msoga = Kikwete
Lushoto = Rip Mkapa
Mjimwema = Mwinyi
Mwitongo = Baba wa Taifa

HUKO MASAKI NANI KASEMA?

HUO NI UHUJUMU WA MALI YA UMMA.
 
Hii ni dharau ya jiwe anatuonesha kipindi hiki ambavyo anaomba kura
 
Acha wivu
 
inaumiza sana....ngoja niishie kukaa kmya
 
Walikuwa na nyumba sasa wanajengewa makasri ambayo pengine hawakuwa nayo kuonyesha utukufu wao!
 
Je wamkumbuka yule rais wa Uruguay?! Kastaafu na kajumba ka kawaida tu na ka gari beetle, na ukumbuke Uruguay ni nchi tajiri kuliko sisi, sasa viongozi wetu lazima wawe na mahekalu kadhaa, magari makubwa kadhaa, ac bank iliyonona, wafanyakazi na vijakazi wakutosha...inasikitisha sana kwa kweli. Kabla ya kujengewa kwani walikuwa wanalala nje?!
Halafu eti tuzidi kuwapa kura wale zaidi?! Hakuna kabisa.
 
Eti watu humu wanakuambia mwenye nacho ndiyo anaongezewa[emoji23][emoji23][emoji23]
Ila siyo haki kabisa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Ningewaona wana Akili kama 'wangetudanganya' kwa kusema Jeshi ndiyo limeamua kuja na 'Utaratibu' huu ila Serikali 'Kukiri' inaleta 'Hoja' nyingi.
 
Wakati ile sheria inaanza utekelezwaji ilikuwa awamu ya Mkapa na ndiyo maana alijengewa baada ya kustaafu akakabidhiwa 2007. Baada ya hapo wakaona kwanini wasimjengee Mzee Mwinyi naye. Mchakato ukaanza pia awamu ya Jakaya ila mradi haukukamilika baada ya Serikali kutotoa pesa kwa wakati na kusababisha mkandarasi kuondoka Site.

Awamu ya Magufuli ndiyo ikaufufua mradi ule ambapo mkandarasi aliyeachia njiani akaleta gharama kubwa mno, Si unajua tena Magufu akasema TBA na Suma JKT walete bajeti zao ambapo makadirio yao yalikuwa chini Tsh. BILIONI 1.1 na ushee kulinganisha na makandarasi wa awali, Suma JKT wakala shavu.

Nina maana kwamba hizi siyo kampeni kivile ile timing ndo imepelekea uone kampeni.
 
Hii ni mojawapo ya sababu LUKUKI za kupigia Lissu kura ili kuwaondosha hawa wanyonyaji WAKOLONI WEUSI.
 

Wabinafsi Marais wenzao wanajali mambo waliyofanya na wanajenga Library za kumbukumbu zao wakati wa uongozi lakini wenzetu wanahitaji wajengewe ikulu za binafsi wakati tayari wana nyumba. Kikwete ana nyumba ya serikali, Mkapa, Magufuli tena kajenga na apartment pale St Peter's. Sasa nyumba za nini? wakati nchi masikini.
 
Yawezekana ikawa ni nia njema tu ya Serikali ila 'Kinachonishangaza' na 'Kunisikitisha' hawa Wote 'wanaojengewa' wana Majumba yao mengi sana.
CCM wamehalalisha wizi wa mali za Umma, mchana kweupe. Aibu sana hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…