Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Maskini katika nchi yetu akihisiwa kutenda kosa au akituhumiwa kutenda kosa viongozi uchukua vyombo vya habari na Polisi kisha kuwachapa adharani. Matukio haya yamefanywa kwa waalimu, mafundi ,wanunuzi wa vyuma chakavu nk
Ukiangalia adhabu hii inavyotolewa ni wazi utagundua inatolewa kwa maskini na watu wasio na watetezi. Tunawizi wa mabilioni unafanywa na wasomi na viongozi waandamizi nchini lakini lakini sijawahi kusikia kiongozi akichapwa kiboko.
Kuna wafanyabiashara wakubwa wanafanya wizi na matendo ya hovyo lakini wakikamatwa awahojiwi bila kuwepo mawakili wao. Si tu KUHOJIWA lakini wanaweza wakakaa kimya hadi mawakili au wawakilishi wanaowaamini wafike ndipo watoe maelezo. Hawachapwi Wala kulazimishwa kimamlaka
Kama tunaamini tunataka kuitumia hii Kama adhabu kwanini tusiwachape Mawaziri, Makati wakuu, wakuu wa Wilaya na Mikoa nk adharani mbele ya camera?
Huu ubaguzi wa mnyonge kuchapwa Kama ng'ombe au punda huku wasomi na viongozi pamoja na familia zao wakipelekwa kwenye vyombo vya sheria tunautoa wapi?
Tunatengeneza Taifa la ubaguzi na lisiloamini katika usawa wa utu pale tunaruhusu viongozi kuchukua sheria mkononi kwa wanyongenambao hata wao Tanzania Ni Mali yao. Kama kweli hawa wanaochapa wanyonge viboko wanaamini wanarekebisha taifa basi wawachape pia viongozi, wafanyabiashara na wasomi/ royal family za nchi hii. UBAGUZI NI SUMU YA USTAWI WA TAIFA.