Tujadili ubora wa magoli ya Simba vs Horoya

Tujadili ubora wa magoli ya Simba vs Horoya

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kutokana na wingi wa magoli, naona hatujapata muda hasa wa kuyazungumzia vizuri ubora wa magoli waliyofunga Simba. Nimeona ni vizuri tulijadili hili.

Kwa upande wangu nitazungumzia hasa magoli mawili.

Goli la 6 ni moja ya magoli bora niliyowahi kuona timu ya Tanzania inafunga. Angalia wingi na ubora wa pasi zilivyokuwa zinapigwa kwa usahihi na kasi kuelekea goli lile na jinsi Chama alivyomalizia. Draft iliyochezwa pale utaiona tu kwa best teams duniani.




Angalia goli la 5 la Jean Baleke. Najua wengi ikiwemo mimi tulikuwa tunaona kama Baleke alikuwa na kauchoyo fulani kutompa mpira Chama apate hat trick pale, na Chama alikuwa anauomba mpira kweli. Nimekuja kuangalia tena, kumbe angempa mpira Chama pale ingekuwa offside na inahitaji umakini mkubwa kwa mchezaji kutambua hilo na kufanya maamuzi magumu. Lakini pia angalia utulivu wa Baleke na jinsi alivyopiga mpira kwenye tight angle lakini akiwa na almost uhakika wa kufunga. Nimeshawahi kusema Baleke anafungaga magoli magumu sana. Baleke ni silent killer!

Kuhusu Denis Kibu. Nashangaa kuna mcha-mbuzi juzi nimemsikia akisema Kibu hakucheza vizuri. Goli la pili lilitokana na shuti kali la Kibu kupanguliwa, mpira ukamfikia Baleke akafunga. Goli la 4 la Kanoute pia lilitokana na shuti la Kibuku kupanguliwa pia ndiyo mpira ukaenda kwa Saido aliyempasia Chama akamsogezea Kanoute. Kibu anacheza mpira sahihi kwa mahitaji ya timu sasa hivi.
 
Lack of capital
Forced labour
Low wages
....
 
Nyuzi za Simba mimi nazipa tuu 😍 😍 😍 😍 😍 😍 ni nzuri zinavutia
Tuliwaacha watambe na nyuzi zao wiki mbili hizi. Walikuwa wamejaza nyuzi za Feitoto na propaganda za kuichafua Simba. Tunafanya kampeni za usafi 😅🤣😂
 
Baleke ali desh kipa akayumba akapiga mahali alikokuwa na uhakika kipa hafiki, goli la chama pia utulivu mkubwa
 
Goli bora kwangu ni goli la kwanza la putin,pale alikopigia mpira bila akili uwezekano wa kupaza mpira ni 97%.ila jamaa alifanya ku press kwa ufundi sana.
 
1679344798537.png
 
Haya sasa. Nimefanikiwa kulipata goli la 6. Nimehesabu pasi zisizopungua 18 hapo bila Horoya kugusa mpira hadi goli. Ila angalia pia accuracy na speed ya pasi zenyewe.


 
Back
Top Bottom