Kutokana na wingi wa magoli, naona hatujapata muda hasa wa kuyazungumzia vizuri ubora wa magoli waliyofunga Simba. Nimeona ni vizuri tulijadili hili.
Kwa upande wangu nitazungumzia hasa magoli mawili.
Goli la 6 ni moja ya magoli bora niliyowahi kuona timu ya Tanzania inafunga. Angalia wingi na ubora wa pasi zilivyokuwa zinapigwa kwa usahihi na kasi kuelekea goli lile na jinsi Chama alivyomalizia. Draft iliyochezwa pale utaiona tu kwa best teams duniani.
Your browser is not able to display this video.
Angalia goli la 5 la Jean Baleke. Najua wengi ikiwemo mimi tulikuwa tunaona kama Baleke alikuwa na kauchoyo fulani kutompa mpira Chama apate hat trick pale, na Chama alikuwa anauomba mpira kweli. Nimekuja kuangalia tena, kumbe angempa mpira Chama pale ingekuwa offside na inahitaji umakini mkubwa kwa mchezaji kutambua hilo na kufanya maamuzi magumu. Lakini pia angalia utulivu wa Baleke na jinsi alivyopiga mpira kwenye tight angle lakini akiwa na almost uhakika wa kufunga. Nimeshawahi kusema Baleke anafungaga magoli magumu sana. Baleke ni silent killer!
Kuhusu Denis Kibu. Nashangaa kuna mcha-mbuzi juzi nimemsikia akisema Kibu hakucheza vizuri. Goli la pili lilitokana na shuti kali la Kibu kupanguliwa, mpira ukamfikia Baleke akafunga. Goli la 4 la Kanoute pia lilitokana na shuti la Kibuku kupanguliwa pia ndiyo mpira ukaenda kwa Saido aliyempasia Chama akamsogezea Kanoute. Kibu anacheza mpira sahihi kwa mahitaji ya timu sasa hivi.
Tuliwaacha watambe na nyuzi zao wiki mbili hizi. Walikuwa wamejaza nyuzi za Feitoto na propaganda za kuichafua Simba. Tunafanya kampeni za usafi π π€£π
Goli bora kwangu ni goli la kwanza la putin,pale alikopigia mpira bila akili uwezekano wa kupaza mpira ni 97%.ila jamaa alifanya ku press kwa ufundi sana.
Haya sasa. Nimefanikiwa kulipata goli la 6. Nimehesabu pasi zisizopungua 18 hapo bila Horoya kugusa mpira hadi goli. Ila angalia pia accuracy na speed ya pasi zenyewe.