Tujadili uhusiano Kati ya t-shirt mpya kuvaliwa juu ya shati chafu na misaada kutumika kupamabana na umasikini tunapoangazia mapokezi ya Mhe. Rais

Tujadili uhusiano Kati ya t-shirt mpya kuvaliwa juu ya shati chafu na misaada kutumika kupamabana na umasikini tunapoangazia mapokezi ya Mhe. Rais

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Nampongeza Mhe. Rais kutamka adharani Kwamba amekwenda ulaya kurejesha mahusiano yaliyoaharibika Kati ya Tanzania na Nchi za Ulaya. Amewaonyesha kamati ya kusifu na kupongeza Kwamba walilitendea vyema tumbo wakaacha Nchi ikiwa na matobo. Pili nimpongeze Kwa juhudi anazofanya, natambua amekuta mfuko wa hazina umepungua sana.

Nirudi kwenye mada, tafsiri ya umaskini wa fikra na Mali nipamoja na kuvaa nguo chafu ndani ya nguo safi. Unaupenda umaskini Hadi unapopata Fedha ubadiliki unaendelea kung'ng'ania umaskini. Leo tumeona kilichokea Uwanja wa ndege; watoto wetu na dada zetu wamefika kumpokea Mhe. Rais wakiwa wamevaa nguo mpya. Wengi wamevaa t-shirt zenye kumbe mbalimbali na Kwa mwonekano zimevaliwa maalim Kwa mapokezi ya Leo. Nimpongeze aliyeshiriki KAZI hii naamini mshahara wake utapanda soon akiwa Mkuu wa mkoa.

Lakini Kuna kosa kubwa limefanyika; Hawa watu wamefika na t-shirt zao wakiwa na waandishi wa habari Kwa ajili ya kuchukua matukio. Nimesikitika kuona asilimia kubwa wamevaa mavazi mapya juu ya mavazi machafu. Hii naamini siyo bahati mbaya, haya nimatokeo ya binadamu kuwafanya wanyonge watumwa. Kumkuta mwendesha bodaboda ukampa t-shirt avae juu ya nguo zake za KAZI ni aina flan ya utumwa. Kumkuta mjasiriamali ukampa t-shirt avae juu ya nguo zake za KAZI ni jambo la fedhea. Kumbukeni wamepiga picha kipindi ambacho Ulaya wanaangalia kama mama kafika salama Tanzania. Next time msiwavalishe nguo juu ya nguo, wapeni wakavalie nyumbani. Natambua mmefanya hivyo kudhibiti wasichukue t-shirt wakatokomea pasipojulikana, lakini mngeweza kuwataftia chumba wakabadilisha Kisha wakavaa nguo zao za KAZI baada ya tukio. Mmefanya Jambo ambalo tusipowaambia mkarekebisha litaathiri wengi. Take it as challenge and next event take time to plan

Lakini nimesema upo uhusiano mkubwa Kati ya kufunika uchafu na nguo safi unapolinganisha kufunika umaskini Kwa misaada. Misaada Duniani kote haiondoi umaskini wa watu, inakusaidia ushibe upate nguvu yakufanya KAZI. Nadhani sisi waswahili wa pwani na mwambao wa Zi kuna usemi tunatumia "USINIPE SAMAKI, NIPE NYAVU NIKAVUE".
Maana yake, USINIPE msaada nikapambane na umaskini Bali nipe Mbinu zakukabiliana na umaskini. Ukijengewa hospitali Kwa msaada ukashindwa kununua dawa na kuweka vifaa tiba ujakabiliana na magonjwa Bali umetengenezewa majengo yakumalizia uhai wa wagonjwa. Ukijengewa Shule Kwa msaada ukashindwa kuisimamia itabaki kuitwa majengo ya Shule. Hivyo nipende kusema kuppkea misaada hakuisaidii Nchi kukabiliana na umaskini.

Kigoma tutajenga airport Kwa msaada, SAWA na Pemba. Then tukimaliza kujenga tunategemea tuutumieje uwanja huo kukabiliana na umaskini? Tumeshawekeza kwenye shirika la ndege lijiendeshe Kwa uwazi na lijisimamie lenyewe? Au tutajenga uwanja ndipo tufufue shirika? Kwanini kigoma na Pemba tusianze na Barabara za lami zitusaidie kufananya biashara yakutupatia faida tututmie faida kujenga uwanja wa ndege wakubeba mizigo na kuwasiadia matajiri waliotokana na ubora wa Barabara?

Hapa tunaposimama navijana waliovaa nguo mpya juu ya nguo chafu au chakavu tukawaambia tumepata misaada ya kukabiliana na umaskini pls tuzitafakari dhana hizi tuone tunatokaje hapa?
1. Tunawezaje kuwaandaa watu wanaokuja kutupokea waje kweli na sura za kutupokea na siyo kuwashawishi waje Kwa wingi wakati nafsini Awana amani na kazi hii?
2. Tunaweza kuwaelimisha wananchi wakatambua Kwamba misaada tunayopewa hauwezi kutufanya tuwe kama Ulaya ila inaweza kutusaidia tufikiri sawasawa Kuhusu matamanio yakuwa watoa misaada siyo wapewa misaada?

Nikiripoti kutoka Murusagamba ni Mimi mwana wa Kamugisha, mchokozi wa mada Kwa ustawi wa Tanzania. Tuishi
 
Kama wamelipwa pesa za watu na wakakubali wavae tu juu ya hizo chafu, unajua Kuna watu niwakuachwa tu hivyo hivyo Bora liende, Kuna mtu ukijaribu kumsaidia anakuumiza hata wewe uliyemsaidia yaani hapo mtu anaona amepata hela ya ghafla akanywe pombe na ujinga mwingine na hayo ndo maisha mpaka kifo hivyo kama ujinga wake haukudhuru ni Bora kuwaacha hivyo hivyo.
 
Back
Top Bottom