Tujadili unga wa lishe wa watoto haijalishi umri

Furahatuu

Senior Member
Joined
Apr 11, 2013
Posts
115
Reaction score
40
Naomba tuchangie hii mada
kuna umuhimu wa kuchanganya nafaka zote sita au hata tano kati ya hizi ? mf ulezi mahindi uwele mtama ngano kwa wakati mmoja wakati wa kuandaa lishe ya mtoto.

nilisikia kwenye tv kipindi fulani dr anasema uchanganyaji huu wa lishe unasababisha uji upikwe kwa muda mrefu hivyo kusababisha baadhi ya virutubisho kwenye huo kupotea.

wadau wanaojua zaidi tuchangie
 
Kwanza kabisa lishe ya mtoto inategemea na umri kuanzia miez6 mpaka8 au9 ni vzr kumpikia nafaka moja kila wiki ili hata kuna yenye aleji kwake ujue ,
Halafu kama utachanganya nafaka zisizid japo kila nafaka ina kaz yake
 
Uwele, mtama hivi vitu najua vinasababisha constipation
nadhani ni vema nafaka zisiwe nyingi
 
muh, mi nachanganya mahindi, mchele, soya, karanga au ufuta, ngano, ulezi, uwele, namtama, japo ukiwa unaanza kwa 6months husiweke mtama, ulezi, wala mawele, weka mahindi, mchele, ngano, na ufuta, wakati wakupika naongeza na maziwa na sukari
 
Kwa mtoto wa miezi 6 mpaka mwaka mmoja inashauriwa usichanganye nafaka bali unaweza saga mahindi peke yake, mchele peke yake, ulezi peke yake, karanga peke yake n.k. Hapo utajikuta una unga wa nafaka mbali mbali na unaweza amua leo kumpikia uji wa mahindi changanya na ulezi kidogo na karanga na maziwa; kesho unaweza amua mpikia uji wa unga wa mchele ili apate ladha ya uji tofauti. Hiyo itamsaidia mtoto asikinai uji. Hapo baadae kama unataka kusaga unga wenye nafaka mbalimbali basi jitahidi usiweke nafaka ya aina moja mfano usiweke mahindi, mchele, ulezi kwani vyote ni jamii ya wanga.
 
Idea nzuri sana hii, ahsante
 
Asilimia kubwa ya nafaka zote ni wanga...mtoto anayeanza kulikizwa ziwa utumbo wake bado haujakomaa kuyeyusha nafaka zote ila pia kumpikia uji wa nafaka moja itasaidia kujua chanzo cha mzio....Wanashauri uji wa nafaka moja na karanga zilizosagwa pembeni anawekewa kidogo uji ukiiva kwa dk 5-10....karanga zina sumu kutu aflatoxins ambayo husababisha kansa ya ini....ila pia hupotea sana kuanzia inaposagwa hadi kupikwa..
 
Karanga zenye sumu ni zile ambazo huwa zna weusi flani ivi na ukiitafuna inakuwa chungu kweli. Kitaalamu inashauriwa ukisaga karanga hakikisha znatumika ndani ya muda mfupi, maana zikikaa mda mrefu huanza kutoa ukungu flani ambao ni
sumu
 
Ni vizuri zaidi tukazingatia ubora wa virutubisho vnavyohitajika kwa makuzi ya mtoto na sio wingi wa nafaka ndani ya lishe. Unaweza tumia nafaka tatu tu, lishe ya mwanao ikawa bora na mwingine akatumia nafaka sita lishe ikawa duni.
 
Nafaka hizo ni zipi?
 
kuna mtu alitengeneza unga wa lishe wa mahindi ya lishe, ngano, uele, mahindi meupe, karanga, ulezi, muhogo, karot. imekaaje hii??
 
Unga mzuri wa Lishe kwa watoto na wa kubwa huu hapa
BOGA,
MAHINDI LISHE,
MTAMA LISHE,
VIAZI LISHE,
KOROSHO AU KARANGA,
ukipenda waweza ongeza na mbegu za mchicha au majani ya mlonge
 
Back
Top Bottom