Idea nzuri sana hii, ahsanteKwa mtoto wa miezi 6 mpaka mwaka mmoja inashauriwa usichanganye nafaka bali unaweza saga mahindi peke yake, mchele peke yake, ulezi peke yake, karanga peke yake n.k. Hapo utajikuta una unga wa nafaka mbali mbali na unaweza amua leo kumpikia uji wa mahindi changanya na ulezi kidogo na karanga na maziwa; kesho unaweza amua mpikia uji wa unga wa mchele ili apate ladha ya uji tofauti. Hiyo itamsaidia mtoto asikinai uji. Hapo baadae kama unataka kusaga unga wenye nafaka mbalimbali basi jitahidi usiweke nafaka ya aina moja mfano usiweke mahindi, mchele, ulezi kwani vyote ni jamii ya wanga.
Asilimia kubwa ya nafaka zote ni wanga...mtoto anayeanza kulikizwa ziwa utumbo wake bado haujakomaa kuyeyusha nafaka zote ila pia kumpikia uji wa nafaka moja itasaidia kujua chanzo cha mzio....Wanashauri uji wa nafaka moja na karanga zilizosagwa pembeni anawekewa kidogo uji ukiiva kwa dk 5-10....karanga zina sumu kutu aflatoxins ambayo husababisha kansa ya ini....ila pia hupotea sana kuanzia inaposagwa hadi kupikwa..
Nafaka hizo ni zipi?Ni vizuri zaidi tukazingatia ubora wa virutubisho vnavyohitajika kwa makuzi ya mtoto na sio wingi wa nafaka ndani ya lishe. Unaweza tumia nafaka tatu tu, lishe ya mwanao ikawa bora na mwingine akatumia nafaka sita lishe ikawa duni.