Tujadiliane biashara zenye faida ya shilingi kwa shilingi

Biashara ya mazao ukiiotea!,Tunanunua gunia la alizeti elfu themanini,mwezi wa kumi na mbili hadi laki2!
 
Nipo kujifunza lakini pia atakaye hitaji kijana wa kumsaidia kwenye kazi zake halali au haramu, nipo hapa. Cha muhimu tu unilipe vizuri.
Vizuri ni shilingi ngapi?🤣
 
Nimefanya na naendelea kufanya biashara tofauti tofauti ila biashara ya vifaa vya simu ukiuza rejareja shilling kuzaa zaidi ya mara mbili ni kitu cha kawaida sana,mfano bidhaa unayonunua elfu 6 kuuza Elfu 18 ni kitu cha kawaida na bidhaa unayonunua Elfu 12 kuuza Elfu 30 ni kitu cha kawaida,imagine protecta unanunua mia tano unauza Elfu 3 hadi Elfu 5 kutokana na sehemu ulipo,biashara zipo nyingi ila zingatia sehemu ambayo bado haina competition kubwa
 
Wow, this is very powerful, Asante sana mkuu umesaidia wengi kwa post hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…