Tujenge Madison Square Tz kwa Ajili Ya Wasanii Wetu.

Tumbo Tumbo

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Posts
1,278
Reaction score
1,553
Wakuu Habari Ya Uzima, Nina Wazo Moja, Tanzania na Dar es Salaam Hatuna Ukumbi Mkubwa Wa Kufanyia Matamasha Makubwa Hasa Burudani Mbali Mbali Kuchukua Nafasi Ya Leaders Club.
.
Sasa Wadau wa Burudani na Sanaa wakiongozwa na BASATA Ikiwapendeza kwa Nn wasikae na Serikali uwapatie eneo popote ikiwezekana kigamboni au mbagala anbapo utajengwa ukumbi ambao utakuwa ni MADISON SQUARE ya Tanzania.
....
Patajengwa kila kitu kinachohusu Sanaa na Burudani zote za kitaifa na kimataifa. SANAA NA BURUDANI NI KIWANDA KIKUBWA SANA CHENYE UTAJIRI NA AJIRA NYINGI.
.....
HIVYO KIWANDA HIKI KITAPATA SEHEMU NZURI YA KUFANYIA KAZI SHUGHULI HASA WORLD CLASS STAGE PERFORMANCE MIAKA YOTE KATIKA UKUMBI WA KISASA.
....
Linaweza kujengwa kwa partnership kati ya serikali kupitia BASATA na Mwekezaji yeyote, Mfano Wachina au Wakorea hasa kupitia cultural institutions zao..... I humbly Submit [emoji120]
 
Kwanini iwe wachina au wakorea? Mi nadhani wabongo ndyo wanapaswa wajenge huo ukumbi coz wanajua nn wabongo wanahitaji
 
Wasanii wetu kwanza wafanye show pale national stadium ili tujue kama Kweli tumefikia hadhi ya kujenga ukumbi kama Madison Square.
 
Naibu rais nilimsikia akisema serikali ikishirikiana na wafaransa wanajenga pale kwenye viwanja vya Tanganyika packers
 
Hao wasanii kwanza Wana msaada gani kwa Jamii

Ova
 
Tanzania ina wasaniii kiasi gani wenye hadhi gani yakupelekea kupoteza muda na pesa kwenye ujenzi huu

Tujadili SGR sio wasanii wasiojielewa
 
Tanzania ina wasaniii kiasi gani wenye hadhi gani yakupelekea kupoteza muda na pesa kwenye ujenzi huu

Tujadili SGR sio wasanii wasiojielewa
Ujinga wa kufikiri ni m-baya sana

Huo ukumbi unajaza wasanii au mashabiki?
Ata wasanii wakiwa wawili, kikubwa ni mashabiki.. Sio lazima wasanii wa ndani tu
 
Tunataka kwanza kanisa kubwa ambalo tutamwabudu Mungu, watu wa imani zote, ili nchi iwe takatifu, mambo yenu ya ufirauni sijui ukumbi wa muziki nendeni kwa mabeberu yanayowatuma, siyo mila zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…