KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Kuna mtazamo ambao umejengeka kwamba Serikali Haina lengo la kutengeneza faida bali kutoa huduma, mtazamo huu Kwa uono wangu hafifu nafikiri ndio chanzo kikubwa Cha baadhi ya mashirika kushindwa kujiendesha na kupelekea kubinafsishwa ama kuingia ubia na sekta binafsi.
Badala ya kuwa na mtazamo wa namna hii kwamba Serikali haipo Kwa ajili ya kutengeneza faida bali kutoa huduma, kwanza kabisa mtazamo huu ubadilishwe, Serikali ianze kujikita katika kutoa huduma na kutengeneza faida.
Serikali iwekeze Kwa lengo la kupata faida kwa namna hii itajikita katika kutoa huduma bora zaidi.
Kwa kufanya hivi, Serikali inaweza ikapunguza Kwa kiasi kikubwa utegemezi wa sera za ubinafsishaji kuendesha mashirika na taasisi zake Kwa kuwa itakuwa ina uwezo wa kuyaendesha yenyewe Kwa faida.