Tujifunze demokrasia kutoka Zambia kama shule

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
279
Reaction score
480
Nchi ya Zambia ilimpata Rais wake wa kwanza mwaka 1968 mzee Kaunda akitokea chama cha UNIP, na baadae wakafuata marais wengine kama 7.
  • Fredrick Chiluba
  • Levy Mwanawasa
  • Rupia Banda
  • Michael Sata
  • Guy Scott
  • Ediger Lungu na
  • Hakainde Hichelema
Zambia tayari inakuwa imebadirisha pia vyama tawala zaidi vya vinne kama
  • UNIP
  • MMD
  • PF
  • UPND
Sasa nataka tujifunze kitu wote bila itikadi, ukisoma historiko na ekonomi ya Zambia kuna mambo ya kushangaza kwa maana ya tulivyo elezwa wakati wa ujio wa vyama vingi. Naomba kuwa juza mnaosoma kuwa Afrika imekuwa na matatizo mengi ya muda mrefu baada ya kuja wageni hivyo jueni kuwa mfumo wa vyama vingi uliletwa pia, na kuambiwa kuwa ndiyo utakuwa muharobaini wa matatizo yetu ya Afrika.

Sasa mpaka mwaka 1988 chini ya Rais Mzee Kaunda huduma ya maji ilikuwa kama bure,
huduma za afya zilikuwa bure, elimu ilikuwa bure na Mzee Keneth alifanya hayo kwa kuuza Kopa na Tumbaku.
Tuliofika Zambia tunajua haya yote sasa ni gharama na mzigo kwa wananchi.
Sasa ukifuatilia kuanzia Chiliba mpaka leo hari inazidi kuwa mbaya na mbaya zaidi vyama vinabadilika viongozi wanabadilika lakini hari sio, tuanze jamani kupunguza hata kidogo imani kwa jamaa zetu waliotwita washenzi.

Swali. Je. Nikweli kuwa mfumo wa vyama vingi umekuwa moharobaini wa matatizo ya nchi za Afrika? Na je umasikini Afrika, vifo, njaa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vimeondoka?

Kwa mawazo yangu mimi kama mtoto wa mchugaji nakataa kabisa kuwa Afriaka hatuweza kuendelea kwa kuletewa maelekezo, mifumo na taratibu kutoka kwa wazungu. Yaani leo hii kilakitu tumeletewa kutoka nje kuanzia Lugha, uvaaji, chakula, sherehe, kuoa, dawa na kuaminishwa kuwa sisi hatukuwa na Mungu ila wao tu ndiyo walikuwa na Mungu na kutuletea dini. Na kibaya zaidi walisema kila kitu chetu kilikuwa cha kishenzi na sisi tukakubari kuwa tulikuwa washenzi.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa kufuata mifumo ya kizungu kwanza ni migumu kwetu na ya uongo ndiyo maana mimi nampongeza Freemani Aikaeli Mbowe na Chama Cha Mapinduzi CCM kwa kushika hatamu kwa muda mrefu madarakani au ofisini, wanafanana kama Marikia Elizabeth wa Uingereza, yeye amekuwapo madarakani tangia mwaka 1952 mpaka leo anamiaka takribani 70 sasa yupo ofisini yule bibi.

Mfumo wetu wa siasa Afrika ulikuwa unafanana na ule wa marikia ndiyo maana Mbowe yupo sahihi kabisa kuwepo ofisini kwa miaka 30 sasa kwani ndiyo asili yetu ya utawala na CCM pia inakaribia miaka 60 madarakani ipo sahihi kwa sababu sisi tulikuwa na viongozi wa Chifudom na Kingdom.
Ninaipongeza sana Chadema, naipongeza CCM na Kingdom ya Muswati kule Eswatini kwani historia yake inafana kingdom ya Uingereza, Japan, Israel, falme ya kiarabu na falme nyingi nyingi duniani.

Nawasilisha mtoto wa mchungaji.
 
Aaaarrghhh!!! Hoja yako ni ipi sasa!! Ccm iendelee kututawala kimabavu!! Hilo haliwezekani. Tunataka Katiba Mpya yenye Tume Huru ya Uchaguzi ili tumshughulikie ipasavyo huyu Mkoloni wetu Mweusi kupitia sanduku la kura.
 
Itoshe kusema kuwa uzi wako umenichefua mchana huu.
 
Hoja zako hazieleweki, umejiandikia andikia tu kama mlevi wa chimpumu.....
 
Ccm inamapungufu yake lkn bado tanzania hakuna chama cha upinzani kilicho tayari
Bado naendelea kuiamini ccm
 
Wazambia wamalawi wananchi wanajielewa
Hawarubuniki ovyoovyo
Wakikutaa wamekukataa

Ova
 
Kwa hiyo Ile Hoja ya kusema tukichagua vyama vya Upinzani kutatokea Vita imekinzana na mfano uloutoa wa Zambia?
 
Nchi ya Zambia ilimpata Rais wake wa kwanza mwaka 1968 mzee Kaunda akitokea chama cha UNIP, na baadae wakafuata marais wengine kama 7.
  • Fredrick Chiluba
  • Levy Mwanawasa
  • Rupia Banda
  • Michael Sata
  • Guy Scott
  • Ediger Lungu na
  • Hakainde Hichelema
Zambia tayari inakuwa imebadirisha pia vyama tawala zaidi vya vinne kama
  • UNIP
  • MMD
  • PF
  • UPND
Sasa nataka tujifunze kitu wote bila itikadi, ukisoma historiko na ekonomi ya Zambia kuna mambo ya kushangaza kwa maana ya tulivyo elezwa wakati wa ujio wa vyama vingi. Naomba kuwa juza mnaosoma kuwa Afrika imekuwa na matatizo mengi ya muda mrefu baada ya kuja wageni hivyo jueni kuwa mfumo wa vyama vingi uliletwa pia, na kuambiwa kuwa ndiyo utakuwa muharobaini wa matatizo yetu ya Afrika.

Sasa mpaka mwaka 1988 chini ya Rais Mzee Kaunda huduma ya maji ilikuwa kama bure,
huduma za afya zilikuwa bure, elimu ilikuwa bure na Mzee Keneth alifanya hayo kwa kuuza Kopa na Tumbaku.
Tuliofika Zambia tunajua haya yote sasa ni gharama na mzigo kwa wananchi.
Sasa ukifuatilia kuanzia Chiliba mpaka leo hari inazidi kuwa mbaya na mbaya zaidi vyama vinabadilika viongozi wanabadilika lakini hari sio, tuanze jamani kupunguza hata kidogo imani kwa jamaa zetu waliotwita washenzi.

Swali. Je. Nikweli kuwa mfumo wa vyama vingi umekuwa moharobaini wa matatizo ya nchi za Afrika? Na je umasikini Afrika, vifo, njaa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vimeondoka?

Kwa mawazo yangu mimi kama mtoto wa mchugaji nakataa kabisa kuwa Afriaka hatuweza kuendelea kwa kuletewa maelekezo, mifumo na taratibu kutoka kwa wazungu. Yaani leo hii kilakitu tumeletewa kutoka nje kuanzia Lugha, uvaaji, chakula, sherehe, kuoa, dawa na kuaminishwa kuwa sisi hatukuwa na Mungu ila wao tu ndiyo walikuwa na Mungu na kutuletea dini. Na kibaya zaidi walisema kila kitu chetu kilikuwa cha kishenzi na sisi tukakubari kuwa tulikuwa washenzi.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa kufuata mifumo y
kwahyo unataka ccm itawale mile au mbowe awe mwenyekiti milele. Hoja zako hazina mashiko.
 
Back
Top Bottom