SoC04 Tujifunze elimu kwa vitendo ili kupata manufaa makubwa ya elimu ya kisasa

SoC04 Tujifunze elimu kwa vitendo ili kupata manufaa makubwa ya elimu ya kisasa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Vincenzo Jr

Platinum Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
24,262
Reaction score
58,728
Elimu yetu inahitaji marekebisho makubwa sana tusiendelee kutoa elimu ya kuchora panzi tu tuendelee kutoa elimu kwa vitendo ili tusiendelee kuwa na vijana wengi waliokosa ajira mitaani.

Nilikua naamka usiku wa manane kuchora hii panzi kwa ajili ya mtihani, ila mpaka sasa sijaona application ya huyu panzi kwenye maisha, au kuna mtu kaona application huko mtaani?

grasshopper_full_610.gif

Chanzo cha picha:Arthropod Morphology: Parts Of A Grasshopper | AMNH.

Hivyo basi ili twende na wakati tunahitaji wizara ya elimu itoke kwenye mfumo wa kuhesabu miguu ya jongoo na kuchora panzi wizara itupe Maarifa, Ujuzi na Kuwa na Mitazamo Chanya Kuhusu Maisha Yetu ya Sasa na baadae
Elimu ya kukaririsha haina msaada Dunia ya sasa.

relativity-pres.jpg

Chanzo cha picha:Relativity Project | schoolspace.gr
20240612_133226.jpg

Chanzo cha picha : The Africa womb Facebook

Hivyo basi tuwekeze nguvu katika mabadiliko haya ili tuwe na elimu nzuri kwa vitendo

Je, ni faida zipi zitapatikana kupitia maboresho haya?
1. Kutatua changamoto za ajira

2. Nchi Itakuwa na wabunifu wengi wakutosha

3. Nchi itapiga hatua masikini watapungua

Hitimisho: Ni vyema tukaangalia Mitaala ya elimu yetu pia Muda wa Wanafunzi kuwa Darasani Kwa Vitendo zaidi Kuliko nadharia hii itawezekana kama Tukiamua mabadiliko
 
Upvote 0
Back
Top Bottom