Tafadhali unapoombwa ushauri na mwana JF mwenzako kupitia post jaribu kutoa replies zenye chanya juu ya hicho kitu alichoomba au msaada anaohitaji kuupata sio kuanza kumuona kama boya fulani yuko nyuma saana kwenye kujua vitu, wengine wareply za kejeli tu hatari, wengine unakuta kaanzisha thread juu ya kitu fulani unaweza kumuuliza swali asikujibu kwa kukiona ulichouliza ni kitu kidogo sana.
Tafadhali tujaribu kuifanya JamiiForums iwe sehemu ya msaada na mchango katika maisha yetu ya kibiashara na mambo mengine nasisitiza maana kuna watu wana majibu kama wamekula weed.
Nashukuruni kama tutakwenda pamoja kwa maendeleo yetu sote