The bump
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,488
- 2,908
1. Heshimu na Mthamini kila Mtu Bila Upendeleo
Tunaona namna gani Tukio la kariakoo lilipotokea waliosaidia wenzao ni wale watu wa kawaida kabisa wa maisha ya kawaida na wala si matajiri au watu wenye uwezo,hii inatoa picha kwamba kwenye maisha Tujifunze kuthaminiana na kuheshimiana.
2.Uwe na Walau Mtu mmoja wa kuweza kumpa maelezo au Maneno ya MWISHO
Ukipita mtandao huko utaona msg za watu waliofukiwa na kifusi kabla hawajaokolewa kila mtu akimtumia ndugu yake/rafiki kumpa maelezo ya mwisho,na wengine kutubu kwa ndugu zao hao,hapa unafundishwa iwe iweje fanya uwezavyo atleast uwe na mtu mmoja unaeweza muachia maelekezo ya nini kifanyike endapo utaondoka na kweli akatimiza.
3.Tusichukue muda mrefu maeneo ya watu na sehemu ambazo sio sehemu zetu za kila siku
Ajali haina hodi wala haikupi taarifa itakukuta wapi lakini binafsi nimejifunza haya maeneo ya watu wengi,mikusanyiko sio salama sana kwani shetani hupenda tumia maeneo hayo kufanya lake.
Masokoni,sehemu za mikusanyiko yoyote,sehemu za starehe,nk hakikisha umeenda kufanya unachofanya ukimaliza sepa zako,Usipoteze muda kukaa maeneo hayo,Kama ni mtu mnakutana muongee jambo Tokeni hayo maeneo tafuteni maeneo tulivu yaliojitenga.
4.Njia ya mbadala ya mawasiliano zaidi ya simu 1
Ukweli kwasasa ukiwa na simu zaidi ya 1 unaonekana kama mshamba au dalali,lakini ukweli ni kwamba Tukio hili la kariakoo waliokua wanatoa taarifa ni wale ambao simu zao zilikua na chaji na wenye simu zaidi ya 1.
Leo kuna mtu katuma ujumbe kasema simu yake kubwa imezima alipo anatumia simu ndogo,Wapendwa simu 1 sio salama tujaribu kumiliki simu zaidi ya 1 kama umeweza miliki smart ya 100,000 hushindwi miliki kisimu cha 20,000, Tujifunze kuwa na simu zaidi ya 1 ina faida nyingi kuliko hasara za kuonekana mshamba.
Na nyie wenye simu 1 basi hakikisheni mnanunua simu zinazokaa na chaji Muda mrefu Majanga hayana hodi.
5.Tuwe tayari kukipokea Kifo wakati wowote
Bado kifo ni tukio ambalo halitokaa tulizoeee kwani linatutenga na watu tulio wapenda bila taarifa,lakini hatuna budi kuwa tayari muda wote,ukitoka nyumbani waage unaowaacha vizuri inatosha sana.
Usiondoke kwenda kutafuta riziki zako ukawaacha watu nyuma hamuelewani,na kwa tunaoishi wenyewe ukitoka unaoweza kuwaaga ni majirani na waliokuzunguka sio kwa kuwagongea milango ukiondoka,ila Jitahidi unapokutana nao asubuhi wakati unaenda kupambana unawasalimia vizuri na kuwatakia siku njema na kazi
njema kisha pita zako.
Tujiweke tayari wakati wote.
Soma Pia: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16