Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Hakika penye wengi pana mengi, kwahiyo tutarajie kukutana na watu wenye tabia tofauti tofauti.
Kuna watu ambao watakukwaza kwa kutokujua na wengine kwa makusudi kabisa, kuna watu ambao furaha yao ni kukuona wewe unakosa raha, kukuona wewe unanung'unika, wanapenda usiwe na amani.
Na njia moja wapo ya kufanikisha malengo yao ni kukuzushia mambo, kukusingizia kwamba umefanya jambo fulani kitu ambacho si kweli na mambo kama hayo.
Ukiingia katika mtego wao kwa kuathirika na njama zao basi hapo utakuwa umewapa ushindi mkubwa na lengo lao litakuwa limetimia, na wataendelea na tabia hiyo mpaka waone umeharibikiwa kabisa.
Kuna namna moja tu ya kujiepusha na Madhira yao na njama zao, nayo si nyingine bali ni kuwapuuza wao na mambo yao.
Kupuuza jambo ni kutolipa uzito au kutolijali na kujifanya kana kwamba halipo au hujalisikia Kabisa, kwa kufanya hivyo halitakuathiri kwa namna moja ama nyingine.
Usitake kuwaonyesha thamani yako kwao kwa kutumia nguvu nyingi kuyapinga yale wanayo kuzushia, tambua wao wanataka kushusha thamani yako iwe jua iwe mvua.
Wafanye wajione wapumbavu kwa kunyamaza kimya, ukimya wako ni majibu tosha kwao kwamba unaitambua thamani yako na wala hutetereki kwa mitazamo yao na vitendo vyao juu yako
Ukimya wako utazima njama zao kwakuwa watakosa nguvu ya kuzidisha mashambulizi kwako kwakuwa wataona kwamba kumbe hauathariki kwa chochote na hivyo kuona wanatwanga Maji kwenye kinu tu.
Binafsi si mshabiki wa King kiba lakini huwa napenda attitude yake, hata asemwe vipi yeye huwa mkimya na mambo yanaishia juu kwa juu tu, na watu wanabaki njia panda kujiuliza je hizi tuhuma ni za kweli au laa.
Hata mashabiki wake wanajua kabisa huyu mwamba hana mambo mengi, utasikia wakisema sijui kama atajibu.
Na wewe pia unaweza kujifunza kuyapuuza mambo na kuwa mkimya, mwanzoni inaweza kuwa ngumu lakini baada ya mda utajikuta unaweza kuyapuuza mambo na kusonga mbele.
Kumbuka maisha ni mafupi mno kuruhusu wapumbavu wachache wakushughulishe.
Ni hayo tu!