Tujifunze kuheshimu utashi wa wengine!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Ipo dhana ambayo imejengwa na baadhi ya wapenzi wa vyama vya siasa, kwa kuwaita machawa, wale wote wanaoonekana kuipenda CCM, kwa mioyo yao.

Watanzania wanauhuru wa kupenda chama chochote cha kisiasa kwa mujibu wa upenzi wa mioyo yao, bila kubughudhiwa wala kuzodolewa.

Kwa wana CCM huwa hawaoni Tabu au nongwa pale wanachadema wanapomsifia kiongozi wao, tofauti kabisa kwa jinsi ambavyo wanachadema wanavyo muona mwana CCM Akimpamba kiongozi wake huku akiwa amejipamba na vazi lake Zuri la kijani kibichi.

N. B,
TUJIFUNZE KUHESHIMU UTASHI WA WENGINE.
#sorry kidogo swahili yangu siyo nzuri sana.
 
Bila shaka wewe ni mmoja wa hao unaowatetea.
 
Ngoja machawa wa vyama vya upinzani waje wakushambulie kwa kusema na wewe ni chawa kama wao!
 
Chawa mna solidarity ya hali ya juu sana.
 
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo kwasasa uchawa a.k.a kujizima data
 
Walijiita wenyewe. Kumbukumbu zipo. Na ni fahari yao kujiita jina lolote. Hawajavunja sheria au kumuudhi mtu. Japo jina Lina sound vibaya.
 
Chawa wana kitu kimoja, "common sense is not common to them"!!

Ukiacha kutumia common sense na kuongea kwa utashi wa wengine kwa jinsi ya kuwafurahisha ili mambo yako yaende, hakuna UTASHI wowote hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…