Tujifunze kupitia Didier Drogba

Enkulu

Member
Joined
Sep 29, 2022
Posts
20
Reaction score
76
Didier Drogba, aliyekuwa mchezaji na mfungaji wa timu ya Chelsea ya mpira wa miguu nchini Uingereza alikwenda mapumziko kwenye hoteli moja ya kifahari iliyoko ufukweni. Aliona magari ya aina zote ya kifahari yakiwa yanaingia hotelini yakiwa yamewabeba mabilionea wakubwa waliokuja kuhudhuria semina.

Semina hizo zilikuwa zinafundisha mada kama vile:

1. Jinsi ya Kujenga Ukwasi Unaodumu Vizazi Vingi

2. Kuelewa Hali na Mazingira ya Kiuchumi ya Afrika

3. Jinsi ya Kufaidi kutokana na mitandao ya Kijamii ili kujenga chapa(brand) inayodumu.

4. Nk.

Mabilionea hawa wanalipa maelfu ya dola za Kimarekani kuhudhuria mafunzo haya. Drogba akawa anajiuliza, kwanini hawa matajiri wanakuja kuhudhuria semina za kuanzia saa chache hadi siku kadhaa?


Kuizima kiu yake ya kutaka kujua, alimwendea bilionea mmoja wa Kiarabu na kumuuliza, "Mkuu, wewe tayari ni bilionea, unahitaji mafunzo haya yote kwaajili ya nini?" Yule bilionea akamjibu, "Mimi nakufahamu, wewe ni Drogba, ulikuwa mfungaji wa Chelsea, je kama mchezaji huwa unaacha kufanya mazoezi na kujifunza kwasababu ya magoli uliyokwisha kufunga?"


Ikaeleweka vyema kabisa! Matajiri huendelea kujifunza na kujiboresha ili kuweza kusimamia na kuukuza ukwasi wao, lakini watu wenye akili ya kimaskini hawaoni umuhimu wa mawazo mapya.


Kila mwaka, Dangote, Tony Elumelu, Mo Dewji, Bakhressa na matajiri wengine unaowafahamu huudhuria kozi mbalimbali. Nilimsikia bilionea mmoja wa biashara akisema kuwa aliwahi kutumia dola za Kimarekani laki moja( $100,000) kwaajili ya kozi maalumu ya wiki moja aliyofundishwa na profesa wa Chuo Kikuu cha Harvard. Hawawezi kuwa vilele kwenye mambo wanayoyafanya bila kuelewa maarifa yanayotawala wakati waliopo. Bustani unayoimwagilia maji ndiyo huwa kijani kibichi.


Asante kwa kusoma.


Imeandikwa na Emmanuel Akyoo
 

Attachments

  • 1723978671283.jpg
    148.2 KB · Views: 5
Most of the celebrities are rich but are not wealthier being rich is what you earn for living being wealthier is what you do with your income that part a lot of people fails.
 
Kwenye hizo course pia unapata contacts, networking, wadau wengine wa wapya kushirikiana nao kbiashara zaidi. Davis wanakutana kila mwaka kubadillisha mawazo.
 
Wamekosa tu shughuli za kufanya hao wanajikeep busy na wanapenda kutupa story za kipumbavu akina sisi ili tuwaone ni wachapa kazi, hivi mnaielewa billion kweli nyie? Ngoja nikupe mfano rahisi;
  • Sekunde millioni moja ni dakika 12.
  • Sekunde billioni moja ni MIAKA 31!
Billionare hana shida yoyote ambayo inahitaji short kozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…