Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Nianze na mfano huu, kuna mtu alikuwa ana umri wa miaka 40's, alikuwa na biashara bahati mbaya ikafa, kwa kupaniki akasema "hakika sasa nitaishi maisha ya shida na familia yangu, na ukiangalia umri umeenda"
Mtu huyu tayar alishaona hana maisha na akaona anguko lake, lakini kiuhalisia ukweli sio huo bali hayo ni maoni yake tu.
Hii ndio hali halisi ambayo tunayo wengi wetu, tunajikuta katika stress za maisha pale tunapokutana na changamoto fulani fulani, na kibaya zaidi jamii yetu imetuaminisha zaidi katika maoni kuliko ukweli,,kwa maana maoni ya mtu au watu ndio tunafanya dira ya maisha yetu.
Tukirudi mfano wa hapo juu, huyo mtu hajui kwamba kuna watu ambao wakifika 50's ndio wanatoboa na wengine hadi 60's bila kumsahau mwanamfalme William amekuwa mfalme akiwa 70's.
Kuna huyu mwanzilishi wa maduka ya KFS,ambayo ni maarufu duniani kote,alikuwa mwanajeshi kama sikosei tena mstaafu,lakini alikuja kutoboa akiwa na miaka 66.
Huyo mwamba badala ya kukaa chini na kujiona ameshafeli maisha,angetakiwa atafute namna ya kupata tena mtaji na kuendelea na biashara zake,,lakini aliamini katika maoni yake kwamba sasa ndo ashakuwa maskini.
Ndugu zangu watu wengi leo tunakatishwa tamaa,kutokana na maoni ya watu,kauli za watu ambazo hazina ushahidi wowote wa kisayansi, au mifano dhahiri,tunajikuta ni watu wa huzuni tu, au tunajiona hatuna nafasi ya kufanikiwa maishani, kitu ambacho si kweli
Kosa letu kubwa ni kuyafanya maoni ya watu au yetu binafsi kuwa ndio ukweli,kitu ambacho sio sahihi kabisa, ni pale tu, tutakapo anza kuyachukualia maoni kama maoni na sio ukweli halisi, hapo tutaanza kuyaona mambo katika namna tofauti kabisa.
Haijalishi una umri gani,maadamu upo hai,basi lolote linawezekana katika maisha,hakuna kuchelewa katika maisha ,ila wakati wako haujafika,trust me. Ukifika utayaona mambo yanakuwa mepesi mno usivyo tarajia.
Iwe unatafuta mtoto,iwe kazi,iwe mume au mke,na jambo lolote lile,amini muda wako utakapo fika kila kitu kitakuwa chepesi kwako, kikubwa subira.
Usiamiani katika maoni ya watu au kauli zao, bali amini katika Mungu na katika ukweli wa mambo.
Ni hayo tu!