Tujifunze kutoka Kenya jinsi Mihimili ya Utawala inavyofanya kazi

Tujifunze kutoka Kenya jinsi Mihimili ya Utawala inavyofanya kazi

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Maandamano ya vijana wa Kenya ya kupinga mswada wa sheria ya kodi 2024/2025 yaliyanza kwa amani, na baadaye yameishia kwenye maafa. Lakini inaelezwa kuwa chanzo ni baada ya Polisi kumwua kijana asiye na kosa, na hivyo kuamsha hasira za waandamanaji.

Vitendo zaidi vya uhalifu vimefanywa na Polisi usiku wa kuamkia jana ambapo Polisi walifanya mauaji ya vijana si chini ya 12, na kuwakamata wengine, baadhi mpaka sasa hawajulikani waliko. Kutokana na Polisi kuzidiwa nguvu na waandamanaji, Serikali iliamua kuwapeleka wanajeshi kusaidiana na Polisi, lakini uamuzi huo umepingwa vikali na Baraza la Maaskofu Katoliki, lililomtaka Rais Ruto kuwarudisha haraka wanajeshi makambini kwao.

Kufuatia vitendo vya Polisi kukiuka katiba, Jaji Mkuu wa Kenya ametoa onyo kali kwa mamlaka zote, ikiwemo Serikali, kuhakikisha hawakiuki katiba, na ametoa wito kwa Wakenya wote kupeleka malalamiko mahakama kuu ya Kenya kama kuna mtu yeyote ametekwa na Polisi, na kuahidi mahakama kufanya kazi hata nje ya masaa ya kazi ili kuwatendea haki waathirika.

Pia soma: Mahakama kuu yaamuru serikali kusitisha zoezi la wanajeshi kwenda mtaani kuzuia maandamo

Kitendo hiki cha Jaji Mkuu wa Kenya kinaonesha uhuru wa mhimili wa mahakama nchini Kenya. Tujiulize kama Jaji Mkuu wa Tanzania anaweza kudiriki kufanya hata 10% ya hiki alichokifanya Jaji Mkuu wa Kenya. Hakika Watanzania katika masuala ya kiutawala bado tupo gizani sana, hata mwanga hatujaanza kuuona.

Ikumbukwe kuwa hakuna nchi hata moja ambayo mambo yote yanaenda na kutendwa kwa 100% perfection, lakini ubora wa mifumo ya utawala inapimwa na uwepo wa mifumo ya kudhibiti waovu na wanaokiuka katiba na sheria. Angalao Kenya wamefika mahali hapo. Kwetu mpaka Rais analalamika juu ya ukiukaji mkubwa wa haki za

1719493982357.jpeg


1719494034852.jpeg



raia unaofanywa na Polisi, ikiwemo mahabusu kuuawa wakiwa mikononi mwa Polisi lakini hakuna anayewajibika wala anayewawahibisha Polisi. Wote tunaishia kulalamika. Sijawahi kumsikia Jaji Mkuu wa Tanzania akikemea ukiukaji wa haki dhidi ya raia unaofanywa na mhimili wa Serikali hata mara moja, japo matukio hayo yapo mengi.

Tangazo la Jaji Mkuu wa Kenya:


Kenya Jaji Mkuu1.jpg
Kenya Jaji Mkuu.jpg
 
IGP kada wa CCM
jaji mkuu Kada wa CCM
Spika wa bunge kada wa CCM

Hapo unategemea nini mkuu kuna watu wanafanya masikhara sana na maisha ya WaTanzania.
 
IGP kada wa CCM
jaji mkuu Kada wa CCM
Spika wa bunge kada wa CCM

Hapo unategemea nini mkuu kuna watu wanafanya masikhara sana na maisha ya WaTanzania.

Nilishangaa sana, miaka michache iliyopita, nilipoambiwa na mtu aliyekuwa kwenye kikao cha chama, akisema kwenye kikao hicho alikuwepo Katibu Mkuu wa Chama, Jaji Mkuu, Spika; kikao ambacho kilikuwa kimeitishwa na katibu mkuu wa chama kwaajili ya kumjadili CAG wa wakati huo. Yaani katibu mkuu anamwita Jaji Mkuu, na jaji mkuu anaenda, tena kwa unyonge!!
 
Nilishangaa sana, miaka michache iliyopita, nilipoambiwa na mtu aliyekuwa kwenye kikao cha chama, akisema kwenye kikao hicho alikuwepo Katibu Mkuu wa Chama, Jaji Mkuu, Spika; kikao ambacho kilikuwa kimeitishwa na katibu mkuu wa chama kwaajili ya kumjadili CAG wa wakati huo. Yaani katibu mkuu anamwita Jaji Mkuu, na jaji mkuu anaenda, tena kwa unyonge!!
Tumekwisha
 
Back
Top Bottom