Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.


Mkuu wewe sio Muafrika? Mbona wajitukana? Tuonyesha ulichofanya tofauti kuhusu hoja hii kuonyesha wenzako ni kima wewe ndio Muafrika pekee?

Mkuu usitukane waafrika wote kwa mapungufu ya wenzao wachache! Ubuntu!
 
Binafsi sina cha kupongeza, wala kushukuru. Maana natambua fika watawala wa CCM ni wabinafsi waliopitiliza! Na kimsingi hawana nia yoyote ile njema na Taifa letu.

Mkuu watawala hutokana na jamii ipi? Sio ya kitanzania? Uwaonavyo watawala ndivyo tulivyo watanzania wote. Hata wewe ukiwekwa pale utakuwa hivyo tu?

Pima tabia ya hawa wafuatao wakiwa nje ya utawala na wakiwa ndani ya utawala utani elewa!

Tuanze na Dr. Slaa, Dr. Molel, Waitara, Katambi, Dr. Bashiru, Motatiro, Kafulila, Shonza na kadhalika.

Mkuu watawala ni true reflection ya jinsi jamii ilivyo!
 
Mkuu wewe sio Muafrika? Mbona wajitukana? Tuonyesha ulichofanya tofauti kuhusu hoja hii kuonyesha wenzako ni kima wewe ndio Muafrika pekee?

Mkuu usitukane waafrika wote kwa mapungufu ya wenzao wachache! Ubuntu!
Sio kama najitukana mkuu hapana, upumbavu wa walio wengi hufanya jamii nzima ionekane niya kipumbavu.mwanafalsa Plato anasema hivi

"Wenye akili timamu wasipo jishughulisha na mambo yanayo husu taifa lao mwisho hutawaliwa na wajinga"

Watanzania tumekubali ( both wenye akili na wasio na akili),kutawaliwa na wajinga hivyo lazima tuvune matumda ya ujinga wetu.

Na wakati huo huo viongozi wenye akili kama Nelson Mandella aliwahi sema hivi

"Ni vema viongozi wajao wa kiafrika kuwa na akili zaidi ya sisi wapigania uhuru,maana yajayo yanahitaji akili na uthubutu"

Angalia viongozi wetu ni aibu ,Kama mtu alipata yai kidato Cha Nne,alafu huyo ndo manager wa kampuni yetu, hiki ni kichekesho Cha Karne.
 
Does this guy’s [Pasko] elevator go all the way to the top?

The amount of drivel he spews leaves a lot of unanswered questions about his state of mind!

Does this guy’s [Pasko] elevator go all the way to the top?

The amount of drivel he spews leaves a lot of unanswered questions about his state of mind!


Mkuu duniani kote kuwa na akili au elimu ya juu hakujawahi kumkomboa mtu kutoka kwenye minyoro ya utumwa/ukoloni wa aina yoyote.

Attributes pekee na zilizothibitika kuleta mabadiliko/ukombozi ni nguvu ya umma, ujasiri na uongozi dhabiti.

Mfano mzuri tazama duniani majeshi yote ya ardhini (infantry) hayana wasomi wa hivyo. Msingi wao ni nguvu ya pamoja, ujasiri na uongozi dhabiti!
 
Katiba mpya na tume huru siyo hisani ni mahitaji yetu kwa sasa. Ushauri wangu ni kwanza tusisubiri mpaka wananchi wazidai kwa njia ya nguvu. Tukisubiri watumie nguvu Wadai hali itakuwa mbaya sana.
Nakumbuka wakati wa mswada wa katiba mpya Kabudi alionya kuwa watanganyika ni watu ambao hawaeleweki kama ilivyo wazanzibari. Wazanzibari msimamo wao unajulikana kwenye mambo mengi. Watanganyika si watu wa kuweka misimamo yao hadharani. Hii ni hatari sana sababu hakuna mtu anajua wanachofikiria kufanya. Naomba nisizungumze zaidi lakini wenye akili wameelewa
 
kwa hiyo unashauri tubaki hivi hivi? Usiangalie katiba mpya kwa ajili ya kukuletea njia muafaka ya kuingia madarakani bali uhitaji kwa maendeleo na usitawi wa nchi
 
Yaani kwamba kamati ya bunge ipokee maoni tofauti na matakwa ya serikali ya chama chao? Ndugu Paskali wewe ni mjuzi sana wa haya mambo usijipe matumaini ambayo hayapo
 
Tusichokijua ni kwamba kila mtu anapigania tumbo ndugu zangu. Watu wanasaka Ulaji nyinyi mnaweka mategemeo hakika mimi nishaachaga huo upuzi kitambo
 
Ni aibu sana kuwa na mwandishi wa habari mwandamizi mwenye mtazamo wa aina hii.
 
Hakuna sehemu ambayo nimeweka wazi kwamba mtu kuwa na Elimu ya juu basi anaondokana na ujinga wake.Mwanafalsa Socrates alikuwa anawashinda kwa hoja Sophists ambao walikuwa wasomi haswa.

Viongozi lazima waandaliwe na watu wenye akili ili waje waongoze kwa akili kubwa hili tunaliona kwa mfalme Philip ii wa Masedonia alimtafutia mtoto wake Alexander the great Mwalimu mwenye akili kubwa na mwanafalsa Aristotle,na mpaka sasa historia ya Alexander the great inasomwa na watu wote duniani.

Mageuzi huletwa na watu wachache wenye akili kubwa,kutengemea mageuzi yataletwa na watu wengi wajinga ni kupoteza muda.
 
Mkuu Pascal Mayalla Tangu jana nimeomba unionyeshe mabadikiko ya hiyo sheria ya Tume ya uchaguzi maana me naona haijabadilika iko sawa japo walichobadilisha ni maneno tu..

Maana yaliyolalamikiwa bado yapo
Kwa mfano bado mkurugenzi ni msimamizi wa Uchaguzi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…