#COVID19 Tujifunze kuyasoma maonyo ya COVID-19

#COVID19 Tujifunze kuyasoma maonyo ya COVID-19

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hulka au Tabia ni jambo la kawaida kwa mtu, taasisi, watu au nchi. Kila mmoja ana yake.

Tangia kuingia kwa ugonjwa huu March 2020 serikali ya Tanzania imekuwa na kigugumizi chake kuuhusu.

Jana waziri wa afya aliingizana stendi ya Magufuli bila hodi:

Waziri mkuu Majaliwa naye alikuwa kivyake Arusha:

Mwenye macho haambiwi tazama.

Taarifa ndiyo hizo, akili vichwani.

COVID-19: India adds Ghana and Tanzania to list of 'at risk' countries - The Financial Express

Penye moshi pana moto.
 
Cotona ni ugonjwa moja wapo kati ya magonjwa mengi yanayodhuru media duniani. Penye media nyingi ndipo corona inadhuru kwa wingi maana wahusika wapo wengi

Namna ya kujikinga

1: Hakikisha unajiepusha na matumizi makubwa ya media

2: zima tv, redio na mitandao ya kijamii katika simu yako muda wote

3: hakikisha hujaingia tweeter ama jamiiforum maana hiyo mitandao ndo chanzo kikubwa cha corona tanzania
 
Cotona ni ugonjwa moja wapo kati ya magonjwa mengi yanayodhuru media duniani. Penye media nyingi ndipo corona inadhuru kwa wingi maana wahusika wapo wengi...
Masahihisho kidogo: Corona haidhuru media, inadhuru hata kuuwa watu.
 
Pengine alimaanisha kuwa tatizo la corona ni propaganda za media zaidi kuliko uhalisia ndiyo maana anasema kujiepusha nao zima TV na media zingine kama Jf

IMG_20211208_075629_531.jpg
 
Uko sahihi.Pengine mtoa mada na wengine wanaoamini corona haipo wataamini siku wakiipata.
Ndugu yangu siyo tu kwamba hatuamini kama corona ipo bali ukweli ni kwamba. Sisi hatuwezi vurugwa na tumafua tu twa kijingajinga kama corona. Iwepo isiwepo kwetu sisi haitutikisi kamwe. Sisi nikisiki cha mpingo bwana corona tushawaachia weupe huko. Labda waunde mpya na waiongeze makali mara kumi zaidi ya hii iliyopo. Sasa wakifanya hivyo wao watabaki salama kama hii tu iliyochini mara 10 ya ile ya kututikisa sisi inawauwa wao. Ukumbuke hata wakiiongeza hiyo mara 10 hiyo itatutikisa tu. Siyo kutuua kama wao!!
 
Labda mwangalie Kipepe hapo aweza kuwa ana kuhusu sana:

#COVID19 - Corona: Wasiochanjwa ni kichocheo kwa Virusi Hatari zaidi

Pia yakitukuta kama hivi tuwe tunaelewa pia:

#COVID19 - Corona: Marekani yaiweka Tanzania katika Mataifa Hatarini
 
Pengine alimaanisha kuwa tatizo la corona ni propaganda za media zaidi kuliko uhalisia ndiyo maana anasema kujiepusha nao zima TV na media zingine kama Jf
Hii ni kweli,media zinachangia sana kuleta taharuki,lakini sio kupuuzia kabisa,huu ugonjwa ni hatari na ukiingia kwenye nyumba yako ndio utajuwa kuwa tahadhari ni muhimu,its life and death,tusilete ukakamavu mbele ya kupambania uhai wako,we only live once..
 
Yaani hizo nyuzi zote hata comment za zenyewe tu zinaonyesha corona si chochote kwetu

Unadhani tunatafuta idadi kubwa ya comments kwenye algebra?

IMG_20211206_195155_472.jpg

Hapa si idadi ya kura mjomba. Wewe tulia sindano ikiungie.
 
Back
Top Bottom