IamMrLiverpool
JF-Expert Member
- Apr 27, 2014
- 4,362
- 6,274
Kutoka Louisville Kentucky nchini. Marekani siku ya jana haikuwa siku nzuri kwa wananchi wa Kentucky baada ya moja ya jengo lililokuwa linajengwa kuporomoka Katikati ya ujenzi.
Kuporomoka huko kuli pelekea mtu mmoja ambaye ni constructor(fundi ujenzi) kufunikwa na kifusi takribani futi 12 kwenda chini. Timu ya uokozi ilifika wakati huo huo na kuanza juhudi za kumuokoa mwenzao, ambacho cha kwanza walichofanya ni kutengeneza mazingira ili yule ndugu aendelee kupumua akiwa huko chini. Masaa 8 baadae timu ya uokoaji ikafanikiwa kumtoa akiwa mzima japo alikuwa na maumivu makali ya viungo.
Mambo ya kujifunza.
1) Baada ya tukio kutokea immediately, Fire team walifika, jamani Kwenye majanga tupeleke timu ya waokoaji badala ya kupeleka wana siasa kwanza. Kentucky kuna meya wa mji na wana siasa wengi tu lakini kwakuwa sio kazi yao kuokoa wala hawa kuwa frontrunners.
2) Kuthamini uhai wa mtu hata kama ni mmoja. Pale Kentucky zimeshushwa magreda, timu ya uokozi karibu 100, na resources nyingine kibao kwa ajili ya kumuokoa binadamu mmoja tu.
3) Kujipanga kwa hali ya juu. Ni kawaida kwa wenzetu kwenye matukio kama haya ambayo yana athiri afya zetu za akili kupatiwa msaada. Baada ya tukio la uokozi yule Bwana yupo hospitali na moja ya huduma anayopewa ni Mental Therapy ili kumuweka sawa kisaikolojia. Sisi unatoka hospitali unaenda Nyumbani utajijua mwenyewe.
Bado tuna safari ndefu sana lakini tuendelee kujifunza kutoka kwa wenzetu.