Nyanda Banka
JF-Expert Member
- Mar 14, 2023
- 304
- 1,054
Pichani ni Nduna Songea Mbano Luwafu. Alipigwa picha hii muda mfupi kabla ya kunyongwa na wajerumani Machi mwaka 1906.
Kifo chake kilitanguliwa na mauaji ya Mashujaa wengine 66 wa Majimaji walionyongwa Februari 27, mwaka 1906.
Songea Mbano alinyongwa pekee yake siku tatu baada ya wenzake hao 66 kunyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja àmbalo lipo katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji katikati ya Mji wa Songea.
Hata hivyo Songea Mbano alizikwa katika kaburi la peke yake.Inasadikika kuwa wajerumani walikata kichwa chake na kuondoka nacho na hapa wamezika kiwiliwili chake tu.
Wazee wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea kila mwaka wamekuwa wanaiomba serikali na Wizara ya Maliasili na utalii kufuatilia kichwa cha Songea nchini Ujerumani ili kiweze kurudishwa Tanzania, jitihada ambazo bado hazijazaa matunda.
Ikumbukwe kuwa Jina la Mji wa Songea limetokana na jina la shujaa huyu mzalendo, ambaye kwayo ustahimilivu wake katika kudai haki ulipelekea kifo chake cha kinyama.
Mwezi Machi mwaka huu tutafanya kumbukizi ya miaka 112 tangu kifo chake kilichotokana na hila za serikali ya kikoloni chini ya Wajerumani.
Hakika ataendelea kukumbukwa daima dumu.