Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
JAPHET KIRILO MTANGANYIKA WA KWANZA KUZUNGUMZA UNO 1952
Katika makala ya nyuma nimemtaja Japhet Kirilo na kuna msomaji kaniandikia na kunieleza kuwa ningemtaja Kirilo kwa sifa ya ushujaa.
Nadhani hakufurahishwa na sentensi yangu niliposema kuwa Kirilo, ''alirejea kutoka UNO mikono mitupu.''
Jibu langu kwake ni hilo hapo chini:
''Oxx,
Japhet Kirilo ni shujaa wetu wala hilo halina wasiwasi na nimeeleza historia yake katika kitabu cha Abdul Sykes.
Japhet Kirilo ndiyo Mtanganyika wa kwanza kuzungumza UNO 1952.
Wakati wa mgogoro wa Land Meru Case Abdul Sykes ndiye alikuwa Secretary and Acting President wa TAA.
Nimekutana na Kirilo ndani ya Nyaraka za Sykes mapema sana kupitia stakabadhi ya fedha alizopelekewa na Mweka Hazina Msaidizi wa TAA Ally Sykes.
Mweka Hazina alikuwa John Rupia.
Fedha hizi alipelekewa Usa River ilikuwa ni Money Order lakini kwa kuwa Usa River hapakuwa na Posta Kirilo hakuweza kuzitoa hizo fedha hapo.
Kirilo yeye akiishi Usa River.
Mwaka wa 1989 nilikwenda nyumbani kwa Japhet Kirilo kumhoji bahati mbaya alikuwa amesafiri.
Fedha hizi alipelekewa kama masurufu ya safari afike Dar es Salaam ili aungane na wanakamati wenzake - Saadan Abdul Kandoro na Abbas Sykes kwa safari ya kutembea kwenye majimbo.
Uongozi wa TAA uliunda kamati hii ya watu watatu kwa nia ya kuwaeleza wananchi dhulma za ukoloni kuwa wanaweza wakachukua ardhi za watu na isiwe chochote.
Lakini kulikuwa na agenda kuu nyuma ambayo Abdul Sykes na viongozi wenzake walikuwa wameipanga nayo ilikuwa kuwatayarisha wananchi majimboni kwa ujio wa TANU waliyokuwa wamekusudia kuunda.
Abdul Sykes alifanyakazi karibu sana na Kirilo chini ya Meru Citizens Union iliyokuwa inashughulika na mgogoro ule na zipo barua ambazo Abdul alikuwa akiandikiana na Sablak wa Meru Citizens Union.
Bahati mbaya huyu mzalendo katika nyaraka anatokea kwa jina moja tu hilo la Sablak.
Abdul Sykes ndiye aliyezungumza na Earle Seaton ili aisaidie Meru Citizens katika kutayarisha, ''petition,'' kwenda UNO, New York.
Earle Seaton alikuwa rafiki wa Abdul Sykes na ndiye aliisaidia TAA kuandika mapendekezo ya mwaka wa 1950 yaliyopelekwa kwa Gavana Edward Twining mapendekezo yaliyotayarishwa na TAA Political Subcommittee.
Waingereza walimnyima Kirilo passport ili asiweze kusafiri na ikabidi Abdul Sykes aingilie kati na mwishowe serikali ilimpa Kirilo passport.
Kamati ya Kirilo, Saadan Abdu Kandoro na Abbas Sykes ilisafiri sehemu nyingi za Tanganyika na kufanya mikutano ya hadhara na ikichangisha fedha pia kwa ajili ya TAA.
Mafanikio makubwa ya kamati hii yalipatikana Kanda ya Ziwa ambako Paul Bomani alihutubia mikutano pamoja na kamati.
Historia hii ya Japhet Kirilo ndilyo iliyomfanya awemo katika waasisi 17 walioasisi TANU mwaka wa 1954.''
Picha wa kwanza kushoto ni Japhet Kirilo kama alivyokuwa mwaka wa 1955, Abbas Sykes, Saadan Abdu Kandoro kushoto kwa Julius Nyerere wengine ni kulia
Iddi Faiz Mafungo wa kwanza kulia, Sheikh Mohamed Ramiyya na mwisho ni Haruna Iddi Taratibu na picha ya mwisho ni kushoto Abdulwahid Ally Sykes na Mwandishi nje ya nyumba ya Japhet Kirilo, Usa River 1989.

Comment