Tujikumbushe: Jasusi mkubwa duniani (Marekani)

Tujikumbushe: Jasusi mkubwa duniani (Marekani)

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Inaonekana kwamba kati ya majanga ya kidiplomasia yaliyoikumba Marekani katika miongo ya hivi karibuni, hayajalizidi janga la hivi sasa ambalo limeikumba nchi hiyo baada ya kijana mmoja wa miaka 30 anayejulikana kwa jina la Edward Snowden kufichua ujasusi mkubwa unaofanywa na Marekani kupitia programu ya kijasusi ya PRISM.

Karibu wiki tatu zilizopita, ajenti huyo wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA alifichua jinsi Marekani inavyofanya ujasusi mkubwa sana katika kona zote za dunia kwa kutumia programu ya PRISM. Tab'an ujasusi wa Marekani kwa mataifa mengine duniani una historia ndefu sana na kwa karne nyingi nchi hiyo imekuwa ikililalamikiwa na mataifa mengine ulimwenguni kwa kufanya ujasusi dhidi ya mataifa hayo na kutoheshimu haki yao ya kujitawala. Pamoja na hayo lakini, ujasusi uliofichuliwa hivi sasa na kijana huyo wa Kimarekani umeushitua kupindukia ulimwengu na unaonekana kama vile ni filamu za hadithi za kubuni na za ki-James Bond.

Swali la kujiuliza hapa ni kuwa, kwa nini ufichuaji huu uliofanywa na Edward Snowden umeushitua vibaya ulimwengu? Kwanza kabisa ni kwamba PRISM ni programu pana sana ya kijasusi ambayo inakusanya na kusambaza taarifa nyingi za kijasusi kwa mkupuo mmoja. Kwa maneno mengine ni kuwa, programu hiyo inakusanya taarifa za mazungumzo ya simu ya watu wote kwenye kona zote za dunia na kupeleka moja kwa moja taarifa hizo kwa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani, NSA. Tab'an kitendo cha shirika la NSA cha kusikiliza mazungumzo ya simu za watu duniani ni jambo ambalo limekuwa likifanyika kwa miaka mingi, lakini kuwafanyia ujasusi watu wanaotumia Intaneti ni jambo jipya lililofichuliwa na Edward Snowden. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, taarifa zote za watumiaji wa Intaneti zikiwemo barua-pepe, chat, mafaili ya sauti, picha na mengineyo yanayopakuliwa kutoka katika Intaneti yanakusanywa na programu hiyo na kutumwa kwa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani NSA.

Jambo hilo lina maana ya kwamba, Marekani imedhibiti miamala yote ya wanadamu duniani kwa ghafla moja. Nukta nyingine katika nyaraka zilizofichuliwa na mfanyakazi huyo wa zamani wa shirika la NSA zinaonyesha kuwa, ujasusi huo wa Marekani haufanywi dhidi ya watuhumiwa wa ujasusi na wakazi wa nchi zenye ugomvi na Marekani tu, bali hata marafiki na waitifaki wa karibu kabisa wa Marekani hawakusalimika na programu hiyo ya kijasusi ya PRISM. Hii ina maana ya kuwa, Marekani inawaangalia watu wote kwa jicho la uadui na shaka. Yaani wananchi wote wa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa ni hatari sana kwa Wamarekani kwa kiwango kile kile cha hatari ya wananchi wa Afghanistan, Pakistan na Yemen kwa nchi hiyo. Sifa nyingine ya programu hiyo ya kijasusi ya PRISM haikuishia tu kwa wananchi wa kawaida bali inawafanyia ujasusi pia viongozi wa ngazi za juu wa nchi za duniani zikiwemo ofisi za Umoja wa Ulaya huko Washington na New York, bali hata katika makao makuu ya umoja huo mjini Brussels, Ubelgiji.

Kukusanya taarifa za siri za viongozi wa nchi na jumuiya za kimataifa kunaipa uwezo serikali ya Washington kuwalazimisha viongozi hao kutii amri za Marekani wakati wowote wanapotaka, vinginevyo viongozi hao wakubali kufedheheshwa na Marekani kupitia kufichuliwa siri zao. Lililo muhimu hapa ni kuwa, Wamarekani hawakukanusha mambo yaliyofichuliwa na Edward Snowden, bali wamekiri kuwepo programu hiyo na wametoa amri ya kutafutwa kimataifa aliyefichua siri hizo. Hii ina maana kwamba Wamarekani hawana nia ya kuachana na ujasusi huo licha ya kufichuliwa kashfa hiyo. Hatari zaidi ni kuwa, Edward Snowden ana nyaraka nyingine za siri ambazo kama zitatangazwa, basi serikali ya Marekani itakumbwa na kashfa nyingine kubwa ya kijasusi.

Chanzo:
Irib World Service
 
edward_snowden_wanted.jpg.1000x297x1.jpg
 
Natamani kukisikia wanachozungumza viongozi wangu wa kitaifa wanapopigiana simu na marais wengine duniani,ikiwamo America,je huwa wanapeana ushauri au wanazungumza nini hasa.!
 
Natamani kukisikia wanachozungumza viongozi wangu wa kitaifa wanapopigiana simu na marais wengine duniani,ikiwamo America,je huwa wanapeana ushauri au wanazungumza nini hasa.![/Qaka nikupebUOTE]

Ukimuomba Snowden utapata taarifa zote unazozihitaji,yupo humu humu JF anaperuzi habari mbalimbali za Dunia,nikiwa fresh nitakupa ID yake umcheki
 
hili baraaa, kwa hiyo mimi walikuwa wananirecord kipindi alikuja bush maana nilikuwa natukana ile..., au hawakuelewa lugha maana nilikuwa natukana kinyamwezitu
 
Aiseeee......
 
hili baraaa, kwa hiyo mimi walikuwa wananirecord kipindi alikuja bush maana nilikuwa natukana ile..., au hawakuelewa lugha maana nilikuwa natukana kinyamwezitu

Hawa jamaa sidhani kama hufuatilia mambo madogo ambayo hayana madhara moja kwa moja kwa Raisi na nchiyao kiujumla.
Pia ili waanze kukufuatilia, lazima pawepo au patokee hali na pengine chochote cha kutia mashaka
 
Inabidi tuwe tunatumia lugha zetu za asili tu!

Lakini kumbuka kwa teknolojia tulio fikia, dunia imekua na mashine zinazo tumika kwa kutafsiri lugha mbali mbali na tofauti pia
 
Lakini kumbuka kwa teknolojia tulio fikia, dunia imekua na mashine zinazo tumika kwa kutafsiri lugha mbali mbali na tofauti pia

Mhh. hizo mashine zinaitwaje mkuu, maana ninavyojua, huwa wanaajiri Agents ambao wanakua fluent kwa lugha mbali mbali
 
Mhh. hizo mashine zinaitwaje mkuu, maana ninavyojua, huwa wanaajiri Agents ambao wanakua fluent kwa lugha mbali mbali

Mkuu nimekuletea mashine bila ajizi.
Sema lingine tafadhali
 
Attachments

  • 1429796413590.jpg
    1429796413590.jpg
    10.9 KB · Views: 683
  • 1429796430087.jpg
    1429796430087.jpg
    10 KB · Views: 599
  • 1429796444256.jpg
    1429796444256.jpg
    7.2 KB · Views: 589
  • 1429796459826.jpg
    1429796459826.jpg
    7.9 KB · Views: 579
Natamani kukisikia wanachozungumza viongozi wangu wa kitaifa wanapopigiana simu na marais wengine duniani,ikiwamo America,je huwa wanapeana ushauri au wanazungumza nini hasa.![/Qaka nikupebUOTE]

Ukimuomba Snowden utapata taarifa zote unazozihitaji,yupo humu humu JF anaperuzi habari mbalimbali za Dunia,nikiwa fresh nitakupa ID yake umcheki

Sure mkuu steveaichi,natamani kujua coz naona taifa uchumi wetu unaporomoka kwa kasi ya ajabu nimeenda bureau de change leo nashangaa $1 inaenda 1947,sasa nataka kujua Kikwete akimpigia simu Obama huwa hata haombagi ushauri jinsi ya kusimamisha uchumi wa taifa lake,hata kama sio Obama basi jirani zetu Kenya hapo,je akimpigia simu Kenyatta huwa wanapiga soga tu au wanapeana skills za kuendesha nchi,nini hasa wanachoongea?ni biashara au nini?@Snowden Tanzania tunakuhitaji tusaidie kujua wanachoongea hawa wahishimiwa.
 
Last edited by a moderator:
Hii kiboko.that is what we call intelligence msemo mmoja unasema "Mtu pekee wa kumuamini katika siri zako ni wewe mwenyewe".

Nahisi hawa jamaa ndo wanafanya hii kitu.me nafikiri iko poa na nifundisho kwa sisi kama binadamu tunaoishi kirafiki leo na kesho kiadui.
 
Ivi wakuu Russia alipona.kweli kweny huu udukuzi!?
 
Ivi wakuu Russia alipona.kweli kweny huu udukuzi!?

Kwa mimi nacho dhani iwe russia,China,Korea au taifa lolote lenye nguvu lina fanya hii kitu sema tuu ni kwa kua Mr.
  • Edward Snowden. kamsemea mmarekani.

    kama tunakumbuka hivi juzi kati tuu mmarekani huyohuyo alikua analalamikia China kua wana Hack baadhi ya Information zao za kibiashara.

    Kesi ipo kwetu tusio weza kutafuta hata Website ya Ze utamu kwa wakati ndo tutapata tabu na hizi mali tulizonazo.ndo watatukamua mpaka tubaki mkia.

Hawa jamaa sidhani kama hufuatilia mambo madogo ambayo hayana madhara moja kwa moja kwa Raisi na nchiyao kiujumla.
Pia ili waanze kukufuatilia, lazima pawepo au patokee hali na pengine chochote cha kutia mashaka

Lakini kumbuka kwa teknolojia tulio fikia, dunia imekua na mashine zinazo tumika kwa kutafsiri lugha mbali mbali na tofauti pia

Wazungu wanajua lugha karibu zote za kienyeji. Nilikuwa nchi moja ya Ulaya sasa siku moja Nikiwa na jamaa fulani wakinaijeria niliokutana nao kule na kuwa marafiki, tulikutana na wazungu fulani waliokuwa wakiongea kiigbo cha kwao, wale jamaa hawakuamini. Huo ni mfano tu, Wanao wataalamu wa farsi, pashto, urdu, kiarabu, kisukuma, sembuse kinyakyusa, kizaramo, kihehe, kiha?
Kuhusu maswala madogo au makubwa, mambo ambayo yanastahili kufuatiliwa, hao watu wanafuatilia mpaka mambo ya kipuuzi ila huyachuja kulingana na mahitaji ya muda huo. Kuna taarifa fulani za kighaidi, ziliwahi kufanyiwa kazi na hao jamaa, baadae zikaonekana kuwa zilikuwa za uongo na ilikuja kugundulika kuwa zilipatikana kwa mtu aliekuwa chooni katika nchi fulani ya Ulaya.
Usiyachukulie mambo kwa wepesi, wewe umeona haya leo, wenzio walishayafikiria miaka mingi nyuma.
 
Sure mkuu steveaichi,natamani kujua coz naona taifa uchumi wetu unaporomoka kwa kasi ya ajabu nimeenda bureau de change leo nashangaa $1 inaenda 1947,sasa nataka kujua Kikwete akimpigia simu Obama huwa hata haombagi ushauri jinsi ya kusimamisha uchumi wa taifa lake,hata kama sio Obama basi jirani zetu Kenya hapo,je akimpigia simu Kenyatta huwa wanapiga soga tu au wanapeana skills za kuendesha nchi,nini hasa wanachoongea?ni biashara au nini?@Snowden Tanzania tunakuhitaji tusaidie kujua wanachoongea hawa wahishimiwa.

Mkuu,nchii hii haina viongozi,masuala kama haya hawajui watayashughulikia vipi,ndio tatizo la kuajiri kwa kujuana bila kuangalia sifa za mtu,sehemu nyeti kama BOT ama Wizara ya Fedha kwa nyadhifa za juu na za kati kama zingelikuwa na watumishi wenye shule ambazo sio za mashaka mashaka,masuala kama haya yasingewashinda kabisa,Mkuu inasikitisha sana,naionea sana huruma nchi yangu na raia wake kiujumla,sijui nikajifiche wapi,1$=Tshs.2000???,huu ni ubakaji Mkubwa sana wa uchumi wa nci yetu,viongozi walio madarakani wanahujumu uchumi wa nchi hii kwa kuwa siwaoni wali siwasikii wakichukua hatua yoyote kuhusu suala hili,sasa sijui wao kama wao wanalichukuliaje suala hili
 
Back
Top Bottom