Tujikumbushe Kidogo

chavalla

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
451
Reaction score
354
[HASHTAG]#FAHAMU[/HASHTAG] Muigizaji wa filamu ya 'God Must be Crazy', Nǃxau ǂToma, alizaliwa mwaka 1944 huko Namibia, ametokea katika jamii ya kabila la 'San'. Katika maisha yake aliwahi kuwaona wazungu watatu tu mpaka pale alipopata bahati ya kuigiza kwenye filamu hiyo, kabla ya hapo alikuwa hajui maana ya pesa na thamani yake wala hajui ilikuwa nini, aliona ni kama kipande cha karatasi, alipolipwa pesa yake kutokana na sanaa ilibidi aelimishwe pesa ni nini, baada ya hapo aliweza kuijengea familia yake nyumba ya tofali, yenye maji na umeme, kwa mujibu wa vyanzo vya Namibia, alikuwa hajui kuhesabu zaidi ya 1-20. Alipata bahati ya kuzunguka nchi mbali mbali duniani kuigiza filamu, baada ya hapo alirudi nyumbani kwake Namibia. Mwaka 2003 alifariki kwa ugonjwa wa TB.

Share na wenzako waweze kumjua 'Bushman'.
 
Ati wanasema anafanana na alikiba!
Kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…