Magufuli alisema Watanzania wanajua kuchambua mambo na lilipotokea tukio la kutekwa kwa Mo zilikuja habari nyingi kwamba waliohusika na utekaji ni Wazungu wa aina fulani lakini suala hilo lilipomalizika liliacha maswali mengi zaidi.
Aliongeza kuwa walijaribu kulichoma moto gari lakini baadaye aliyetekwa akaonekana anakunywa chai na kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.