Tujikumbushe maneno aliyoyasema Patrick Aussems( Uchebe) alivyoondoka Simba

political monger senior

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2020
Posts
1,827
Reaction score
5,994
Disemba 3,2019 aliyewahi kuwa kocha wa Simba Patrick Aussems aliandika ujumbe wa kuwashukuru na kuwaaga wapenzi na mashabiki wa Simba na Watanzania kwa ujumla kwa wakati wote waliokuwa pamoja baada ya kufutwa kazi na klabu hiyo.

Sehemu ya ujumbe wake Aussems maarufu UCHEBE aliweka na ushauri usemao,

''Ili simba ikue ni lazima iwaondoe kabisa Viongozi waongo na watu wasio na elimu kwenye bodi''

Huenda ulikuwa ni ujumbe uliochukuliwa poa lakini kwa haya yanayoendelea sasa ya mashabiki na wapenzi kushinikiza mitandaoni baadhi ya viongozi wa juu wa klabu kuachia ngazi moja kwa moja linatukumbusha ujumbe wa Aussems ile Disemba 2019.

Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.

 
Huyu walimuonea wakamuondoa bila sababu yoyote ya msingi, aliifanya Simba Sc ikacheza mpira mzuri sana, nikikumbuka mpira tuliocheza tukiwafunga Nkana 3-1 kwa Mkapa tukaingia makundi ya Klabu Bingwa Afrika, na game nyingine tukawafunga Vita Club ya Congo, pale ndipo Simba ilikuwa haswa kwenye ubora wake.

Aussems alitengeneza mpaka wachezaji vijana wakawa tishio, alikuwepo Miraji Athuman super sub matata sana, kila akiingia uwanjani anafunga, leo hata sifahamu kijana yuko wapi, yote haya ni kwasababu ya ujuaji wa Mo. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa haya majanga yanayotukuta sasa, kila kocha anayekuja hamalizi miaka miwili.
 
denooJ hii I'd yako?
 
Matatizo ya simba ni kuanzia.
1. Muwekezaji.
2. Mwenyekiti mangungu.
3.Try again.
4. Body ya wakurugenzi
5. Management.
6.Benchi la ufundi lote.
7. Scout analyst,nk
8. wadau.
9. Washauri wa Bodi.
10 mashabiki mbumbumbu
Akitolewa chama wanalia na kuzomea pmf sana, wanamlilia miquisson kurejeshwa, Adebagor na manzoki
 
Afrika matatizo ni yale yale tokea enzi za kina Mwenemutapa...
1. Lack of good leadership
2. Civil wars with societies
3. Installation of puppets
.
.
.
.
etc
 
Rashid Juma kijana mdogo aliaminiwa na angekuwepo leo hii angekuwa mchezaji mkubwa sana ila makocha waliokuja nyuma yake walikuwa wanapanga wachezaji kwa kukariri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…