Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,346
Kwa wanaokumbuka, Kenya ilikuwa na mchakato wa katiba kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2002.
KANU wakitumia wingi wao bungeni walilazimisha kuandikwa kwa rasimu mbovu ambayo ilipingwa na vyama vyote vya upinzani wakati ule. Walipoenda kwenye kura ya maoni, "wapinzani mahasimu"; Raila na Kibaki walijikuta katika kundi moja la Orange lililokuwa likipinga rasimu ile.
Matokeo ya kura ya maoni yalishuhudia kundi la orange likishinda na rasimu ile kutupiliwa mbali. Wapinzani kwa kuona matunda ya kuungana kwao waliendeleza umoja wao na ndipo Raila alipotamka, katika uwanja wa Kasarani kuwa "Kibali tosha"... akimaanisha kwa mara ya kwanza Mjaluo anaungana na Mkikuyu. Mafanikio ya ushindi katika kura ya maoni yalipelekea wapinzani kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2002. Je, kuungana kwa wapinzani wa kweli Tz katika mchakato wa katiba, itakuwa chachu ya kuwaunganisha na kushinda uchaguzi mkuu ujao?...
Kwenu wachambuzi