Tujikumbushe, ni kitu gani kimewahi kukutoa ushamba!?

Kichangiri

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
331
Reaction score
675
Nianze mimi mwenyewe
Siku ya kwanza nimeingia kwenye kituo cha mwendokasi aisee sitokaa niisahau. Baada ya kupewa tiketi kwenye kuiscan ile tiketi palinitoa jasho. Akanisaidia dada mmoja mrembo sana. Kwenye kuingia sasa nilijikuta nanyanyua lile chuma nkidhani linafungukia juu nikakaa hapo dakika moja nzima hadi nkaona wa pembeni yangu kaingia. Ilibidi nisubiri kituoni ndani hadi nihakikishe wote walioniona wamepanda magari na kuondoka ndipo na mimi nikapanda

Embu tushirikishane ni kipi kimewahi kukutoa ushamba hutokisahau?
 
Zile mashine za kupitisha tiketi kwenye mwendokasi hadi leo zinanisumbua aisee... na scan kumbe haijasoma unataka kupita unakuta chuma halizunguki.
 
Last edited:
Mie kilichowahi nitoa ushamba nilinunua blenda ya kusagia matunda / viungo sasa imefika siku nataka kuanza kuitumia kwa kusaga viungo vya chai nikaifunga ile blenda kumbe haiwezi kusaga mpaka ukaze mara tatu ambapo ile ya tatu unatumia nguvu kidogo ili ipate kuwaka. Basi huwezi amini nikahangaika wee kumbe naishia sehemu ya pili kila nikiwasha inagoma si nikajua Mhindi kanipiga basi nikaibeba blenda kurudisha kwa Mhindi tena nina hasira hapo sababu niliinunua bei kidogo mpaka nafika ananielekeza namna ya kuifunga duuh niliona aibu sana aisee sababu duka lilikuwa limejaa wateja hapo lol.

Kutoka hapo nikabaki najicheka tu kwani nimetoka ushamba kwa kitu kidogo.
 
Ni vingi kweli kweli.

Kwanza TV.
Nyumbani imekuja TV nabonyeza tu button bila kuelewa nikajikuta nimeweka Lugha ya kichina. Nikaona hamna anayeniona nikazima nikajikausha, watu wamehangaika mpaka wakasoma manual wakairudisha.

LIFT/ ELEVATOR
Mara ya kwanza kupanda lift ilipoanza kuondoka nilihisi kichwa kama kinapata mgandamizo miguu inatetema nikajikuta nimejishikilia sehemu hivi ili nisianguke. Na sikujua namna ya kuioperate so nikashuka floor ya yule mtu kisha nikaendelea kupanda juu kwa ngazi.

NGAZI ZA QUALITY CENTRE/ ESCALATORS
Naweka mguu bado kidogo nile mweleka mguu mmoja ukabaki juu mwingine upo chini halafu nikawa nimejishikilia kwenye kingo. Washkaji walicheka sana na ile komedi
 
Escalator/Ngazi inayotembea.
Mpaka sasa mimi na huyo jamaa ni maadui wa kudumu, sijawahi kumzoea na sitaki kumzoea.
siku ya kwanza nilishikiliwa kama vile mbuzi akiwa hataki kwenda anavyovutwa aisee ilikua hatari.
 
Mkuu umeyisha
 
Naingia benki mara ya kwanza baada ya kufungua mlango na kuingia naona mlango unarudi wenyewe sasa nikaogopa usije kujibamiza kwasababu ni wa kioo nkaushika na kuuanza kuupeleka taratibu .

Mlinzi ndo akanambia hauna shida we achia tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…