stanluva
Senior Member
- Apr 7, 2009
- 153
- 33
Na kumbuka Mabweni ya Urafiki, umoja, maendeleo, ujamaa na muungano!
- Nakumbuka shida ya umeme iliyokuwa itokea na kulazimika kutumia chemli!
- Kama mtakumbuka Kuna kisima cha kupampu a.k.a Shadufu! Aisee kilitoa msaada wa kutosha katika kutupa maji ila ndo kuoga watu ilikuwa issue passport kama kawa!
- Pia kulikuwa na huduma ya mihogo "mayau/mayao au makaba" ya kuchemsha kila asubuhi wakati wa uji "pola" ya kiuzwa na wamama wa vijijini toka Mletele!
- Nakumbuka library yetu ilivyokuwa imechoka ukiingia utakuta vitabu vya hadithi za Abunuasi na adili na nduguze! Vitabu vya taaluma iliku vya enzi zile za 67! Dah ilikuwa shughuli kama kulikuwa na assignment!
- Kwa wale wapenzi wa disco mnawakumbuka tamsala/ Tamso "Songea Girls" Mwanangu ilikuwa lazima Uoge na Pafyum!
- Nakumbuka mitaa ya Ulokoni {vijijini} kulikuwa na mama mmoja maarufu kama binti bull huyo mama dah ni noma kila service unapata chakula na vingine pia!
- Bila kusahau Kuchunga Ng'ombe wa shule na kulima mashamba ya shule dah ilikuwa kazi kwelikweli kwa sisi watoto wa ocean road jembe hatukuwahi kulishika zaidi ya kusomakwenye vitabu!
- Namkumbuka mwl. mmoja muhohela vijana walikuwa awakimwita maps da alikuwa ni noma ni zaidi ya Feudal wa Tosa Huyu alikuwa capability ya ajabu ya kukutambua akiwa umempa mgongo kisha ukiwa na bifu naye duu utajuta!
- Bila kusahau umbali uliopo toka mjini hadi shule {4KM} lakini dah wazee tulikuwa tunachapa kwa mguu unaweza kwenda na kurudi mara mbili au zaidi! Lakini leo tunapanda gari fire na kushukia bahkresa kariakoo!