Kizimkazimkuu
JF-Expert Member
- Nov 8, 2007
- 337
- 240
Mi nazikumbuka hizi
Mariam
Nakonda kama mnazi kwa mapenzi niliyonayo,
Jina lako nakuota mchana kutwa sili ee
Moyo wanichechemea, mwili damu kauka eee
...na hiki kipande, katika Mola nalilia mtoto
Nakulilia mola wangu eee
Nakuwaza mola wangu eee eh
Yaliyonikuta ni makubwa naona haya
Mbona nateseka,
Karibuni mnaozikumbuka tungo za nguli huyu aliyetutoka 2010.....
MUZIKI ASILI YAKE WAPI
WIMBO NISEME NINI
SIKU YA KIFO
NAPENDA pia KAROLA, MREMA, NARUDI NYUMBANI, SAUTI YA MNYONGE, HARUSI YA MWANZA
[NALILIA MTOTO - Matimila]
Nakulilia Mola wangu weee,
Nakuwaza Mola wangu wee,
Yalonipata makubwa naona balaa,
Wala hamu sina x2
Wenzangu wana watoto,
Mimi sina hata wa dawa eeeh,
Niwatumapo wana wa wenzangu,
Mama zao hunisimanga x2
Nalia nasikitika bahati sina,
Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,
Mola, Mola, Molaaa eeeh,
Mola eeeh nataka mtoto,
Mola Mola, Molaa eeh,
Mola eeh, nalilia mtoto
Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!
Mola Mola, Mola eeeh....
[MWANAIDI - Matimila]
(Kibao MWANAIDI kilipigwa na wana Matimila enzi hizo.
Sauti ni za Skassy Kasambula, Kyanga Songa, Fan fan na solo
ni la Batii Osenga bila kumsahau Mbwana Cox katika rythim)
nimetokea kumpenda binti Mwanaidi
nimeridhishwa na tabia yake
nikaamua tufunge nae pingu za maisha
urithi ulioacha baba niliutumia
ili kuneemesha ukoo wake
nilianza kuuza mifugo
hatimaye shamba
ili kumtosholeza mahitaji yake ehhh
baada ya miezi michache nikapata barua kutoka kwa Mwanaidi
..... .. kuwa yeye hanitaki tena
tena hawezi kuolewa na mimi
(wote)
mimi najuta eh najuta mama
gharama nilizogharamia
ameona bure
sijui la kufanya .. nasikitika oh
sababu yako ....... Mwanaidi x 3
SAUTI YA MNYONGE
Mama yeh yeh yeh yeeeh
Mama ninalia weh
Mama uko wapi
Mama nateseka eh
Mama umejificha wapi
Mama yoh yoh yoh yoh yoh yohoooo...
Mama mi nalia ohooo
Mama mi nalia eheee
Mama mi nalia
Ninalia ohooo
Mama uko wapi
Mama weh
Mama uko wapi ohoo
Remmy analia eheee
Mama uko wapi ohoo
Uko wapi ohoo
Mimi mtoto yatima
Sina baba wala mama
Sina dada wala kaka
Sina ndugu mwenzenu
Sina ndugu mwenzenu ehee
Nikaombe kwa nani ihiii
Niende wapi
Najutia ulimwengu
Nimekosa nini mola
Unyimwa ndugu
Nikazaliwa peke yangu
Mwenzenu sina baba wala mama
Sina shangazi wala mjomba
Sina babu wala bibi
Niende wapi ohoo
Niende wapi eheee
Jamani niende wapi
Masomoni nimefukuzwa
Nalikuwa sina sare
Nalikuwa sina viatu
Nalikuwa sina madaftari
Nimekwenda eh kwa mwalimu mkuu
Mwalimu nihurumie ehee mwalimu
Baba yangu ni kiwete eheee
Mama yangu ni kipofu mwalimu
Madaftari nani ataninunulia mwalimu ehee
Unapinga kunisikiliza oh mwalimu
Amenifukuza kiroho mbaya
Shauri ya unyonge eh
Sababu ya unyonge
Sababu ya unyonge ehee
Niende wapi ohoo
Nimekwenda kuomba kazi nikaambiwa sina kisomo
Nimeuza machungwa nipate kula nikaambiwa sina kibali
Nimeuza big g nikaambiwa mimi mzururaji
Nimeuza sigara nikaambiwa mimi mlanguzi jamani
Sijui nile wapi ohooo
Jamani nile wapi eheee
Nikaombe kwa nani
Kijijini nimefika nikaambiwa mimi ni mwizi
Ngedere kala mahindi nikaambiwa ni mimi
Nguruwe kala mihogo nikasingiziwa ni mimi
Jirani akiibiwa naambiwa ni mimi jamani
Sijui niishi wapi ohooo
Jamani niishi wapi eheee
Uko kijijini nakoishi hakuna bia
Uko kijijjini nakolima hakuna stoo ya soda
Sasa uniambie ninywe nini ehee
Jamani naomba kinywaji ninywe gongo
Gongo pombe ya wanyonge ehe
Gongo pombe ya wakulima
Nikinywa gongo nalima kama punda
Nikinywa gongo nalima kama farasi
Hiyo nyanya unanunua kariakoo unajua inatoka wapi
Kwa sisi walevi wa gongo uko kijijini
Sisi ndio tunanguvu ya kulima
Jamani nasikitika ehee
Niende wapi ohooo
Jamani niende wapi ohooo
Mimi sikusoma
Hata ulaya wazungu wengine hawakusoma
Sisi wote tukisoma
Nani atamsomesha mwenzie
Jamani nanyanyaswa ohoo
Niende wapi ehee
Jamani niende wapi ohoo
Sikupendelea nizaliwe kilema
Sikutaka kabisa nizaliwe kipofu
Nikiomba msininyime ehee
Nikipita msinicheke ehee
Mimi mtoto yatima
Pia ni mukulima
Nyumba nalijenga ya makuti
Nalalia ngozi la mbuzi
Chini kuna viroboto ohooo
Pia kuna kunguni ihiii
Jamani sina umeme ehee
Naishi kwa kibatari
Sina chandaruha
Hata kidonge ya klorokwini nyumbani kwangu sina
Naishi kimungu mungu
Naogopa ukimwi
Niende wapi ohooo
Wenye nguvu mnawajua vizuri
Matembezi yao ni kwa gari
Starehe zao kilimanjaro
Ukienda kilimanjaro sasa hivi utawakuta
Wake zao wamepaka lipstiki wazuri kama malaika
Watoto zao wote wanasoma ulaya
Niambie mimi mkulima jamani
Mwanangu shuleni amefukuzwa
Mke wangu anavyaa midabwada
Mimi mwenyewe sina pesa jamani
Niende wapi ohooo
Jamani niende wapi eheee
Nikaombe kwa nani
Mama yoh yoh yoh yoh
Mama ninalia weh
Mama uko wapi
Mama nateseka ohooo....
Mama yeh yeh yeh yeeeh
Baba ninalia weh
Baba uko wapi
Baba nateseka eh
Baba umejificha wapi
Mama yoh yoh yoh yoh yoh yohoooo...
Mama mi nalia eheee
Remmy analia ohooo
Masikini remmy analia ohooo remmy weh
Remmy ni mnyonge ehe
SAUTI YA MNYONGE
Mama yeh yeh yeh yeeeh
Mama ninalia weh
Mama uko wapi
Mama nateseka eh
Mama umejificha wapi
Mama yoh yoh yoh yoh yoh yohoooo...
Mama mi nalia ohooo
Mama mi nalia eheee
Mama mi nalia
Ninalia ohooo
Mama uko wapi
Mama weh
Mama uko wapi ohoo
Remmy analia eheee
Mama uko wapi ohoo
Uko wapi ohoo
Mimi mtoto yatima
Sina baba wala mama
Sina dada wala kaka
Sina ndugu mwenzenu
Sina ndugu mwenzenu ehee
Nikaombe kwa nani ihiii
Niende wapi
Najutia ulimwengu
Nimekosa nini mola
Unyimwa ndugu
Nikazaliwa peke yangu
Mwenzenu sina baba wala mama
Sina shangazi wala mjomba
Sina babu wala bibi
Niende wapi ohoo
Niende wapi eheee
Jamani niende wapi
Masomoni nimefukuzwa
Nalikuwa sina sare
Nalikuwa sina viatu
Nalikuwa sina madaftari
Nimekwenda eh kwa mwalimu mkuu
Mwalimu nihurumie ehee mwalimu
Baba yangu ni kiwete eheee
Mama yangu ni kipofu mwalimu
Madaftari nani ataninunulia mwalimu ehee
Unapinga kunisikiliza oh mwalimu
Amenifukuza kiroho mbaya
Shauri ya unyonge eh
Sababu ya unyonge
Sababu ya unyonge ehee
Niende wapi ohoo
Nimekwenda kuomba kazi nikaambiwa sina kisomo
Nimeuza machungwa nipate kula nikaambiwa sina kibali
Nimeuza big g nikaambiwa mimi mzururaji
Nimeuza sigara nikaambiwa mimi mlanguzi jamani
Sijui nile wapi ohooo
Jamani nile wapi eheee
Nikaombe kwa nani
Kijijini nimefika nikaambiwa mimi ni mwizi
Ngedere kala mahindi nikaambiwa ni mimi
Nguruwe kala mihogo nikasingiziwa ni mimi
Jirani akiibiwa naambiwa ni mimi jamani
Sijui niishi wapi ohooo
Jamani niishi wapi eheee
Uko kijijini nakoishi hakuna bia
Uko kijijjini nakolima hakuna stoo ya soda
Sasa uniambie ninywe nini ehee
Jamani naomba kinywaji ninywe gongo
Gongo pombe ya wanyonge ehe
Gongo pombe ya wakulima
Nikinywa gongo nalima kama punda
Nikinywa gongo nalima kama farasi
Hiyo nyanya unanunua kariakoo unajua inatoka wapi
Kwa sisi walevi wa gongo uko kijijini
Sisi ndio tunanguvu ya kulima
Jamani nasikitika ehee
Niende wapi ohooo
Jamani niende wapi ohooo
Mimi sikusoma
Hata ulaya wazungu wengine hawakusoma
Sisi wote tukisoma
Nani atamsomesha mwenzie
Jamani nanyanyaswa ohoo
Niende wapi ehee
Jamani niende wapi ohoo
Sikupendelea nizaliwe kilema
Sikutaka kabisa nizaliwe kipofu
Nikiomba msininyime ehee
Nikipita msinicheke ehee
Mimi mtoto yatima
Pia ni mukulima
Nyumba nalijenga ya makuti
Nalalia ngozi la mbuzi
Chini kuna viroboto ohooo
Pia kuna kunguni ihiii
Jamani sina umeme ehee
Naishi kwa kibatari
Sina chandaruha
Hata kidonge ya klorokwini nyumbani kwangu sina
Naishi kimungu mungu
Naogopa ukimwi
Niende wapi ohooo
Wenye nguvu mnawajua vizuri
Matembezi yao ni kwa gari
Starehe zao kilimanjaro
Ukienda kilimanjaro sasa hivi utawakuta
Wake zao wamepaka lipstiki wazuri kama malaika
Watoto zao wote wanasoma ulaya
Niambie mimi mkulima jamani
Mwanangu shuleni amefukuzwa
Mke wangu anavyaa midabwada
Mimi mwenyewe sina pesa jamani
Niende wapi ohooo
Jamani niende wapi eheee
Nikaombe kwa nani
Mama yoh yoh yoh yoh
Mama ninalia weh
Mama uko wapi
Mama nateseka ohooo....
Mama yeh yeh yeh yeeeh
Baba ninalia weh
Baba uko wapi
Baba nateseka eh
Baba umejificha wapi
Mama yoh yoh yoh yoh yoh yohoooo...
Mama mi nalia eheee
Remmy analia ohooo
Masikini remmy analia ohooo remmy weh
Remmy ni mnyonge ehe